Friday 22 September 2017

HADITHI PICHA 09: DADA VUA

..........ilipoishia

HUKU KWA KINA HELENA MAMBO YALIKUWA HIVI:-
Sule alivizia taratibu kuingia ndani ili achukue lile begi lake ili aendelee na safari yake.Kweli alifanikiwa kuingia ndani lakini alishangaa kuona begi lake zipu ilifungwa nusu.Kumbe Lucy alivyokutwa na Shangazi yake alilifunga haraka haraka hakulifunga vizuri,Basi alichungulia ndani ya begi akakuta picha zake ziko juu juu wakati aliziweka chini kabisa.Kwa kuwa alishaharibu kule hakutaka kuremba alifunga begi lake kisha akatoka kwa kunyata,Lakini kumbe Lucy hakuwa mbali sana na nyumba.Sule alimuona Luchy akiwa amemkamatia mbuzi kama vile anamchinja,Sule alipigwa butwaa kwani ni kitendo kigeni kwake kuona mwanamke anachinja.Katika harakati za kushangaa Mara Lucy si akamuona Lucy alimtupia bonge ya tabasamu huku mkononi akiwa amekamata kisu kile alichokitumia kumchinja Mbuzi yule......

Pengine kilikuwa ni kitendo cha kushangaza lakini Lucy hakuwa na njia nyingine tofauti na kumuacha mbuzi ajifie lakiƱi hakutaka kuona mbuzi anakufa hivi hivi kwani ni kitoweo.Basi baada ya Lucy kumuona Sule,Lucy alichanganyikiwa kwani alishampenda sana Sule.Lakini Sule hakutaka kabisa mazoea na binti huyu kwani ana kihere here balaa isitoshe ameshakinukisha kule kisimani.Sule alimpungia mkono Lucy ishara ya kumuaga,Lucy alisimama na kumuacha mbuzi pale chini alikuwa bado hajamchinja.Lucy alikiachia kisu pale chini kisha taaratibu akawa anamfuata Kidume Sule"Bright ndio unakwenda"Aliuliza Lucy huku akiumauma kucha zake......"ndio mi nakwenda na usiniite Bright naomba niite Sule".

Huku kisimani palikuwa hapatoshi kwani Shangazi alimcharukia sana Helena"Hivi weeweeee!! umeanza lini tabia ya kupapatikia wanaume!? au nikurudishe vile ulivyokuwa sema umbwa weye"Helena alionekana kulia kwani Shangaziye alimtishia kumrudisha alivyokuwa mwanzo,Basi helena aliongea huku akilia kwa uchungu sana"Haaapana shangazi naomba usinirudishe bora unipe adhabu yoyote nitaifanya".

KWA UFUPI SHANGAZI YAKE NA HELENA NI MCHAWI SANA ANASIFIKA KWA UCHAWI ENEO HILO ANALOISHI.SASA HAPA NDIO UTAJUA HUYU HELENA NI NANI.TWENDE KAZI

Sasa Shangazi alimwambia Helena"Laiti ungejua huyu uliyekuwa naye ni nani usingethubutu kufanya ujinga huu uliokuwa unaufanya".Helena Alimtolea macho shangazi yake hukuakimuuliza"Una maana gani kusema hivyo!??".Shangazi alimjibu"Hupaswi kujua hata kidogo".Shangazi aliongea huku akimnyooshea Helena kidole machoni,Helena baada ya kuona vile alimsogelea Shangazi yake huku analia alishajua baada ya kunyooshewa kidole nini kinafuata"Jamani shangazi nimekuomba usinifanyie hivyo!!!Nisaaamehe shangazi yaaangu!!!"Shangazi huyu ana roho ya kinyama na haogopi kufanya chochote kwani huyu helena na Lucy ni misukule yake na maumbo yao halisi siyo hayo yanayoenekana bali wana maumbo ya kutisha sana,Shangazi aliongea"Si unaringia hili umbo lako sasa unarudi kwenye umbo lako tuone utamringia nani".Helena akizingatia jinsi alivyompenda Sule aliwaza hatamuona tena na hatoweza hata kumkumbatia,Moyo wake ulisononeka sana kwanini sawa na kufa huku ukimuona akupendaye mbele yako anakulilia,Maumivu aliyoyapata hayasimuliki kwa maneno.Basi Helena haikuchukua muda alibadilika na kuwa dubwasha la ajabu sana.Shangazi aliliamuru dubwasha hilo likamzuie Sule asiondoke kwani ana kazi na mtu huyo.

Huku nyumbani aliko Lucy sasa ilikuwa ni balaa,Lucy alimfikia kwa karibu kabisa Sule huku akiongea"Sasa wewe kaka mbona hujiongezi jamouny,Naomba basi uje unisaidie kuchinja huyu mbuzi maana anaumwa na atakufa muda si mrefu"Ilikuwa ni akili ya Lucy ikiweweseka njia ya kumakamata Sule kwani alionyesha dhahiri kumpenda,Sule aliwaza "mmmmh! hapana huyu Lucy atafanya nikutwe tena na Shangaziye hapa halafu ije iwe tafrani"Hapana wacha niondoke,Lakini wakati huo Shangazi yake Helena Alikuwa akizungumza na mizimu yake,Aliongea maneno yake pale akitaka mizimu imstopishe Sule asiondoke kabisa.Sasa Sule hakujua kuwa amejipeleka kwenye nyumba ya kishetani,Mara Sulealishangaa anabadili mawazo badala ya kuondoka akajikuta anaanza kumtamani sana Lucy.

Basi Sule naye alijikuta anamfuata Lucy ili amsaidie kuchinja mbuzi yule.Lucy alijihisi malkia kwani kitendo cha kumshawishi Sule kilizidi kumpa moyo ya kuwa kile alichokusudia kitafanikiwa.Basi Sule alipo maliza kumchinja mbuzi alimtundika tayari kabisa kumchuna.Lucy Alizidi kupagawa na kumtamani Sule kwani habari za sule alizipata kupitia picha na kondom alizozifuma kwenye begi.Basi Lucy alianza tena kumsemsha Sule" Hiiivi!! wee kaka mbona uko siriaz kiasi hicho!!?"......."Niko siriaz kivipi yaani,Si umeniomba nikusaidie na hapa nafanya nini au niache!!?"..........Lucy aliiremba sauti wakati huo yu karibu kabisa na Sule"Hapana Suye simaanishi hivyo"Aliongea Lucy huku akionekana kumvizia Sule kwa nyuma ili amkumbatie.Sule akiwa hana hili wala lile alishtuka kwani alihisi joto limeongezeka kwa mgongoni,Mara alisikia kitu laini kimemgusa.Kilikuwa ni kifua cha Lucy na mikono akiipeleka pale mbele kwenye tumbo la Sule.Wakati hayo yanaendelea Helena akiwaamebadishwa maumbile hakuwa mbali na eneo lile.......Unafikiri nini kitatokea hapo!!!!?Usikose episod inayofuata