Tuesday 26 September 2017

Picha: Pharell Williams aungana na mastaa wengine kupiga magoti

Mwanamuziki Pharell Williams ameungana na mastaa kama J.Cole, Steve Wonder na wachezaji wa timu ya (NFL)National Football Leagu kwa kupiga magoti ikiwa kama ishara ya kulaani tukio la mauaji liliotokea mwezi Agosti maeneo ya Charlottesville nchini Marekani.



Pharell alipiga magoti baada ya kumaliza kutoa burudani katika tamasha la Global Citizens Festival lililofanyika mjini New York, siku ya Jumamosi na kusema kuwa “I’m in Virginia right now, I’m home. Can’t nobody tell me what to do if I want to get on my knees right now.”

Ikiwa na maana hii “Napiga magoti hapa, napiga kwa ajili ya watu wangu, Napiga kwa ajili ya mji wangu, napiga kwa ajili ya bendera ya America inayopepea hapa.”

Siku hiyo ilikuwa maalum ya kuliombea Taifa la Marekani linaloongozwa na Rais Donald Trump, ambapo watu mbalimbali walipiga magoti ‘Take a Knee’.