Friday 22 September 2017

Usiogope kuanza upya – Jux

Baada ya kukumbwa na janga la bomoa bomoa kwenye maduka yake yaliyokuwa maeneo ya Sinza Legho jijini Dar es salaam, hatimae msanii wa Bongo Fleva, Jux amewataarifu mashabiki na wateja wake kuwa tayari bidhaa zake za African Boy zinarudi madukani tena baada ya kukosekana kwa muda.

Jux

Jux amesema anawashukuru sana wateja wake kwa kuwa wavumilivu huku akiwaahidi kutangaza maeneo ambayo bidhaa zake zitaanza kupatikana muda mfupi ujao.

“Nashukuru sana kwa uvumilivu mlioonyesha! Poleni sana kwa kusubiri ! Hivi karibuni nitawapa location lilipo Duka jipya na utajipatia bidhaa zote za #Africanboy na nyingine nyingi! Hakika unaweza kuanguka na ukanyanyuka na kuanza upya,“ameandika Jux kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiwaasa mashabiki wake kutokukata tamaa kwa kila jambo wanalolifanya.


“Hakuna kukata tamaa kila Jambo linawezekana ukimtanguliza Mungu na kupambana! Usiogope kuanza upya,“ameandika Jux.