Friday 22 September 2017

Mambosasa: Tunaendelea kufanikiwa kupunguza Uhalifu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limeendelea kuwa na mafanikio katika kipindi hiki cha operesheni mbalimbali kwani limeweza kupunguzu matukio ya uhalifu yanayoendelea kutokea jiji hapa.

Hayo yameelezwa na kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa alipozungumza na waandishi wa habari leo na kusema kuwa wamefanikia kumkamata Robson Issack miaka 21 mwanafunzi wa IFM mkazi wa Tabata Segerea akiwa na Bastola aina ya Beretta yenye no. DAA 316502 ikiwa na risasi sita ndani ya magazini.

Hivyo baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kushirikiana na rafiki yake aitwaye Patrick Kilosa katika kukodisha silaha hiyo kwa wahalifu kwa nia ya kujipatia kipato. Ufuatiliaji ulifanyika na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye ana miaka 22 mwanafunzi wa chuo cha Columbus State Community cha nchini Marekani, mkazi wa Tabata hivyo wote wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi.

Aidha jeshi la polisi likiwa doria katika eneo la Mbezi jirani na Chuo Kikuu cha Saint Joseph askari walilitilia mashaka gari no. T 364 DJV aina ya Noah rangi nyeupe na kulikamata ndani kukiwa watu wawili Athuman Peter a.k.a Ngosha miaka 44 mfanyabiashara mkazi wa Kivule na Mustapha Hassani miaka 22 fundi seremala mkazi wa Kimara Mwisho wote wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Katika oparesheni hiyo ambayo ni endelevu ya kutokomeza uhalifu jeshi lilifanikiwa kukamata jumla ya Kete 1,591 za bangi , Puli zikiwa 259, Misokoto ya Bhangi 78 pamoja na pombe haramu ya gongo lita 1,479 mitambo 14 ya kutengeneza pombe haramu gongo zote zimekamatwa.

''Oparesheni hii kali ya kuwasaka wahalifu wa makosa hayo mbalimbali ni endelevu na hivyo raia wema wanaombwa kuendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa Jeshi la Polisi ili kurahisisha kukamatwa kwa wahalifu hao na hatua kali za kisheria zifuate dhidi yao ili kupunguza uhalifu wa makosa hayo'' amsema. Hivyo watuhumiwa wote bado wanaendelea kuhojiwa kulingana na makosa yao na pindi upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

Hata hivyo kamanda Mambosasa alieza mafanikio yaliyopatikana tangu tarehe 19 septemba kupitia kikosi cha usalama barabarani wamekusanya zaidi ya Tsh 339,510,000 /= kama toza za makosa ya barabarani ikihusisha vyombo vya usafiri na kusema kuwa bado opereshi hiyo inaendelea.