Monday 25 September 2017

Ripoti: Kundi la P-Square lagawanyika

Kundi la muziki linalowakutanisha ndugu Peter na Paul maarufu kama P-Square limeripotiwa kugawanyika.


Kundi hilo lililofanya kazi kwa zaidi ya miaka mitano linadaiwa kuvunjika rasmi baada ya wawili hao kuingia katika mgogoro mpya. Ripoti iliyowasilishwa na mwanasheria Festus Keyamo kutoka kwa Peter imeonyesha malalamiko kadhaa kwa kundi hilo akiwemo na meneja wao ambaye ni kaka yake Jude.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa Peter amekuwa akimshawishi kaka yake(Paul) wafanye kazi lakini kaka yake amekuwa akitoa ushirikiano hafifu pia imeongeza kuwa, Paul alikatisha tamasha lao lilokuwa lifanyike Amerika Kaskazini.

Vilevile ripoti imeongeza kuwa Paul amekuwa akiwatumia ujumbe wa vitisho kwa familia yake katika mitandao ya kijamii pia meneja kundi hilo ambaye ni kaka yao Jude Okoye aliwahi kumtishia Lola kumpiga bastola.

Kutokana na ripoti iliyotolewa na Peter kupitia kwa mwanasheria wake, Peter amesema imetosha na hawezi kuendelea kufanya kazi sehemu kama hiyo hivyo ameamua kufanya kazi mwenyewe kama Mr P.