Saturday 23 September 2017

Hizi ndio picha za video mpya ya staa wa Bongo Flava anayetikisa Marekani

Babbi ni msanii ambaye anauwakilisha vizuri muziki wa Bongo Flava pande za nchini Marekani. Msanii huyo mpaka sasa tayari ameshaachia ngoma takribani nne huku moja kati ya hizo ndio hajaachia video yake.



Jumamosi hii Babbi anatarajia kuachia video ya ngoma yake mpya iitwayo ‘Kikomando’ ambayo ameitengeneza nchini humo. Hizi ni baadhi ya picha ambazo zitaweza kuonekana katika video hiyo.