Tuesday 26 September 2017

Cheche ya Ommy Dimpoz haikamatiki YouTube


Angalau kwa sasa Ommy Dimpoz anaweza akapumzika baada ya kuutua mzigo mzito wa lawama kutoka kwa mashabiki wake kuhusu kuchelewa kutoka kwa video ya wimbo wake mpya ‘Cheche’.


Hata hivyo hali hiyo inaweza ikawa ni neema kwa msanii huyo kutokana na mashabiki kutamani kuiona kwa muda mrefu. Video hiyo imefanikiwa kushika namba moja kwenye trending ya mtandao wa YouTube na kuzipiga chini video nyingine zilizouteka mtandao huo ikiwemo ‘Seduce Me’ ya Alikiba, ‘Zilipendwa’ ya WCB na ‘Unaibiwa’ ya Rayvanny.


Wakati huo huo, Cheche imefanikiwa kutazamwa mara 121,998 katika siku moja tangu ilipowekwa kwenye mtandao huo.