Friday 27 June 2014

HII NDIYO ATHARI KUBWA KWA WANA NDOA KUKOSA UZAZI.. SOMA HAPA

Kukosa uzazi huweza kuathiri ndoa katika njia nyingi, hii ni pamoja na kuweza hata kufikia hatua mume na mke kutengana na kwa upande mwingine huweza kusababisha mume na mke kuwa na bond imara kuliko kawaida.
Je, kukosa uzazi huweza kuathiri wanandoa kivipi? Kutounganishwa ki-emotions: Hii hutokana na ile hali ya mwanandoa mmoja kutaka kuongea kutoa hisia zake au kuongea kile anapenda na mwingine kushindwa kumwelewa mwenzake na kuhisi hamjali.

 Kutokana na tatizo lililopo wanandoa hujikuta wapo disconnected katika hisia zao na kama mwanaume ndiye mwenye tatizo wakati mwingine inakuwa ngumu zaidi kuongelea kwani wanaume (wachache) huwa wabishi linapokuja suala la uzazi.

 Suala la gharama (Pesa). Kulipia gharama za kimatibabu kuhusiana na suala la kukosa uzazi (infertility) kama vile IVF (in vitro fertilization) kufanya vipimo huweza kutikisa sana ndoa yoyote iliyo imara na wanandoa huiweza kujikuta wakiwa na mzigo wa deni wakati hata mimba haijatungwa bado. Huwa ni jambo la busara kujadili pamoja mke na mume ni namna gani wanaweza kufikia makubaliano wapi pesa zitapatikana na watalipa vipi. 
Tofauti ya malengo ya maisha Inawezekana mmoja kati ya wanandoa ambao wanatatizo la infertility anapenda kuwa na mtoto tena ile ya kupindukia na kama ni mwanaume wengine hali huwa tete kabisa katika ndoa. Utofauti wa mitazamo huweza kuleta friction kubwa hata hivyo kuwa mume na mke ni pamoja na kukubaliana malengo ya maisha na kuimarisha bond ya ndoa.

 Hata hivyo siyo tatizo la kukosa uzazi ndilo hudhoofisha ndoa bali jinsi unavyokabiliana na tatizo la kukosa uzazi ndicho kinachoweza kudhoofisha ndoa yako. Kwanza kubali na kujikubali kwamba hii ni njia ndefu katika maisha na utaweza kukabiliana nayo.

Kubali kwamba unaweza kuishi maisha
marefu kabla ya kupata watoto. Hukuolewa au kuoa ili upate watoto bali kuwa na maisha pamoja na mwenzi wako katika hali zote hadi kifo kitakapowatenganisha na watoto ni matokeo au zawadi kutoka kwa Mungu na ipo siku Mungu atatimiza ahadi yake kwako kwani Mungu si mwanadamu. 
Kuna wakati mmoja wenu au wote kwa pamoja mnaweza kupata habari zinazokatisha tamaa kutokana na tatizo lililopo, jambo la msingi ni kila mmoja kumsikiliza mwenzake ili kuhakikisha anajikisikia vizuri katika feelings zake. Kuwa msikilizaji mzuri wa hisia za mwenzako, usitegemee mwenzi wako atasoma akili yako na kujua unahitaji kitu gani ni vizuri kila mmoja kujieleza vizuri kwa mwenzake anahitaji kitu gani kuliko kubaki kimya na baadae kuanza kulalamika kwamba hakujali.

 Ni vizuri kuishi kwa kuridhika na kile kilichopo kuliko kuishia kwa kuangalia kile ambacho kinakosekana kwenye ndoa au mahusiano yenu. Kuwa na muda wa pamoja na
kufurahia kwa pamoja furaha ya ndoa huweza kutoa ahueni kutokana na tatizo la kukosa uzazi. 
Weka mipaka Kama wazazi wako au ndugu zako wanapenda sana kuingilia ndoa kwa namna ambayo inaonesha kunaweza kuzua mgogoro zaidi ni muhimu kuwa makini kuweka mipaka ya uhakika. Wanaume wengi ikitokea mke anashindwa kupata mimba wazazi wao au ndugu huja juu hata kumshauri kijana wao achane na huyo mwanamke.

Mwanaume lazima usimame imara kuhakikisha unamlinda mke na kuzidi kumpenda kwa kuhakikisha mnakuwa kitu kimoja.