Wednesday 25 June 2014

KANUNI MUHIMU KWA WANAWAKE: FAHAMU UMUHIMUWAKO KWA MWANAMME SI CHUMBANI TUU


KANUNI MUHIMU KWA WANAWAKE
(1)        Kuwa mwanamke ambaye anahitajiwa na mwanaume na sio mwanamke anayehitaji mwanaume.
Tafsiri yake
Kibaologia ubongo wa mwanaume una tofauti kubwa ukilinganisha na wa mwanamke na hivyo utendaji wao na mahitaji
yao yana utofauti pia. Uwezo wa kuzungumza wa mwanamke ni mkubwa kuliko wa mwanaume, yaani kwa siku moja mwanamke ana uwezo wa kuongea maneno 20,000 wakati mwanaume
ana uwezo wa kuongea maneno 7,000 kwa siku. Mwanamke asipojua njia za kuoanisha tofauti hizi atamchukiza mwanaume bila ya yeye kujua na ndio maana Biblia inasema “kila mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake. Bali aliyempumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe (Mithali 14:1).Ili uweze kuwa mwanamke ambaye mwanaume anamhitaji inakupasa usome mahitaji ya mwanaume vizuri ili uweze kuyatimiza kikamilifu na kumtosheleza kabisa.
(2)        Mwanaume akikuacha au kukudharau ni hasara yake na sio yako.
Tafsiri yake
Iwapo una uhakika wa kuifuata vizuri kanuni ya kwanza na kwa bahati mbaya ukapata mwanaume asieuona uthamani wako usibabaike kabisa. Yeye ndie kipofu haoni thamani yako na kuandoka kwake toka katika maisha yako maana yake Mungu anakuelekeza kwa mwanaume mwingine aliye bora kuliko huyo. Biblia inakuagiza “Tulia ujue ya kuwa mimi ni Mungu nitatukuzwa katika mataifa” Zaburi 46:10.
(3)        Onekana kama kipepeo lakini ng’ata kama nyuki.
Tafsiri yake
Biblia inasema kwamba wanawake wanapaswa wajipambe kwa utu wa moyoni usioonekana yaani roho ya upole na utulivu na hekima (Petro 3:4).Mwanamke pamoja na mapambo yote na uzuri wa nje ni muhimu tabia yake ionyeshe utulivu na upole. Kipepeo haumizi mtu na anapendeza kwa muonekano wake lakini hivyo peke yake haitoshi kuvuta na kutunza penzi la mwanaume. Hivyo basi ni muhimu mwanamke mara nyingine awe kama nyuki, yaani aonyeshe ukali pale anapoonelewa. Ajenge uwezo wa kuelezea hisia zake bila ya uoga wowote ule.KUMBUKA kuwa wanaume hupenda wanawake wanaoleta changamoto zinazojenga na sio wenye unafiki.
Kwa kufanya hivyo ataweza kudumisha penzi katika msingi wa haki na ukweli na sio unafiki. Fuata maneno ya BWANA YESU “kuweni na busara kama nyoka  na wapole kama njiwa (Mt 10:16).
(4)        Usianzishe ugomvi bali zifahamu njia za kumaliza ugomvi
Tafsiri
Ukiwa mpole utapenda sana kutafuta kumwelewa mwenzio badala ya kumhukumu ,ukimhukumu hasira huja haraka na hivyo kuanzisha ugomvi. Epuka kukurupuka na kusema maneno harakaharaka .Jifunze kutulia japo umeumia au kukasirika. Kwa kufanya hivyo utaweza kuona kwa urahisi
USIPITWE SOMA HII>>LADIES:Mambo 14 Yatakayomfanya Mwanaume Akuache.
njia za kujibu na kutatua migogoro katika mahusiano yako.  
(5)        Kuwa mpenzi na sio mpiganaji lakini siku zote pigania unachokipenda
Tafsiri
Unapoamua kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu jitahidi kumpa mapenzi yote kwa moyo wote. Pamoja na hayo yote yatokeapo magumu kuwa mstaarabu kuepuka hali ya ugomvi kwa kujizuia kupaza sauti au kuongea maneno makali. Jambo la msingi tambua mambo muhimu na usikubali mpenzi wako ayapuuzie mambo hayo kwa urahisi. Jenga hoja nzito za kupigania haki yako ya kuishi maisha ya furaha na amani.
(6)        Kupata kitu ambacho hujawahi kukipata ni lazima ufanye vitu ambavyo hujawahi kufanya.
Tafsiri
Ni rahisi sana kufanya vitu ulivyozoea na kufurahia hali hiyo mpaka pale itakapotokea shida fulani  inayohusiana na kitu
SOMA NA HII>>UKIMUONA HAMU IMEZIDI SANA BASI FANYA HAYA KUMPUNGUZA
ulichokizoea .Ili uweze kuendelea kufurahia uhusiano wako zaidi ni muhimu utafute vitu vipya vyakupamba na kuimarisha uhusiano wako. Hapa inahitaji ubunifu, uchunguzi na ujasiri wa kujaribu jambo ambalo hujawahi kukutana nalo. Kwa kuwa kila siku tunakutana na mambo mengi upo uwezekano mkubwa wa mtu kubadili mtazamo wake juu yako na ukapata matatizo katika uhusiano wako. Kuleta vitu vipya huleta msisimko mkubwa na iwapo wewe ndio utakuwa chanzo cha msisimko huo basi utathaminiwa na kupendwa zaidi.
(7)        Kabla hujauliza kwanini fulani hakupendi, jiulize kwanini unajali sana juu ya hilo
Tafsiri
Kumpenda mtu mwingine ni kitu rahisi sana na sisi wote tumo katika kundi hilo lakini kumfanya mtu mwingine akupende  au aendelee kukupenda sio rahisi kabisa.Pale unapotamani mtu fulani akupende kwanza jiangalie mwenyewe vizuri je kama mtu huyo anapenda mtu mwenye maumbile mazuri unayo sifa hiyo?. Kama anapenda mtu mfupi wewe unayo sifa hiyo? Na kama anataka mtu mwenye elimu au mwenye pesa wewe umo kwenye kundi hilo.? Hayo yanaweza kuwa maswali magumu kwa wengi lakini swali lingine rahisi kwa kila mtu ni je ni kwa vipi mimi nitaweza kuchangia furaha yake zaidi ya mtu mwingine yoyote?. Ukiweza kujibu swali hili unanafasi kubwa ya kujisogeza kwake na yeye akakuona kuwa kweli unafaa, lakini ukijisogeza bila kuwa na sifa za kutosha unatafuta maumivu ya moyo. Madhaifu kama aibu, hasira, woga, unene kupita kiasi, uvivu au kupenda kuongea bila ya kuchoka yanaweza kuharibu penzi hata kama utapata mtu mwenye penzi la kweli. Jichunguze kama vile Biblia isemavyo.“ Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na angalia asianguke (1Wakorintho 10:12)

“Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani, jithibitisheni wenyewe (2 Wakorintho 13:5).