Thursday 26 June 2014

FAHAMU DALILI ZA MUME ANAETEMBEA KIMAPENZI NA HOUSE GIRL (dada wa kazi)

DALILI YA KWANZA
Ishara ya kwanza ya mwanaume ambaye tayari
yupo ndani ya uhusiano wa kimapenzi na
msichana wa kazi ni kupenda sababu za
kumwamsha mfanyakazi huyo  hata pale
anaporudi na kumkuta amelala.
Utakuta baba amerudi nyumbani usiku wa saa
sita, mkewe anamfungulia mlango, akishaingia na


kukaa, anaanza:
“Dada amelala?”
Mke: “Ndiyo.”
Baba: “Mwamshe nimpe kazi f’lani.”
Mke unaweza ukamtetea sana msichana, lakini
mumeo akasimamia msimamo ule ule.
Sasa utakapomwamsha, akifika, mumeo
utamuona anavyojipinduapindua.
“Hii mboga umepika wewe dada?”
“Hapana, mama.”
“Ooo. Ulifua zile soksi zangu?”
“Ndiyo baba.”
“Sawa kalale.”
Mke unajiuliza, sasa kumwamsha kote kule ndiyo
maswali yenyewe hayo tu.
Sasa tuendelee…
Katika hali kama hii, wewe mke jaribu kuwa
makini sana. Hakikisha hutoi nafasi kwa mumeo
kumfikia au kuwasiliana na hausigeli kwa kitu
chochote. Kama ni maji ya kuoga tenga wewe,
vitu ambavyo vinawezekana kufanywa na wewe
vitimize ili kuukata uhusiano hata kama utakuwa
hujathibitisha kama upo!
Tatizo kubwa ni kwamba, wanawake wengi siku
hizi wanawafanya wasichana wa kazi ndiyo
wenye nyumba, wao wasaidizi, wakati zamani,
hausigeli ndiye msaidizi wa kazi za ndani, mambo
mengine yote ni kwa akina mama wenyewe.
DALILI YA PILI
Ishara hii inatakiwa mke mwenye utambuzi sana,
yaani awe na ufahamu wa hali ya juu vinginevyo
anaweza kukurupuka na kumbwatukia mumewe
kumbe hana habari na msichana wa kazi.
Ila kwa wale ambao wana uhusiano sasa,
ukimwona mumeo ana tabia ya kuchelewa kulala
eti yupo sebuleni, mke changamka, hapo pana
jambo.
Mume anayefanya hivyo hutoa nafasi kwa mkewe
kwenda kulala na yeye kunyatia chumbani kwa
hausigeli kuduu naye.
Sasa endapo mke utakwenda sebuleni na
kumkuta mumeo anajifanya kukodolea macho
tivii ili ujue anaangalia vipindi, jaribu na wewe
kuchunguza aina ya kipindi, ukikuta ni taarifa ya
habari ya Sky News,CCTV, CNN, BBC au Al
Jazeera, ujue huyo mwongo tu, hana lolote.
Lakini usiishie hapo, jifanye na wewe unakaa
pembeni yake kuangalia taarifa hiyo ya habari.
Utamuona yeye anasimama na kusema…
“Tukalale mke wangu.”
Kama wakati wa kwenda kulala wewe
utatangulia, yeye lazima aingie chooni kwanza,
anajifanya anajisaidia haja ndogo lakini
anachotaka ni wewe uingie chumbani, yeye
aingie kwa hausigeli ili ampige busu japo moja
tu, maana anajua dili limeshatibuka.
Lakini dalili hii ni kwa mume ambaye hapo
nyuma hakuwa na tabia ya kukaa sebuleni peke
yake na kuangalia tivii.
Kwa upande wa hausigeli aliye katika uhusiano
na baba mwenye nyumba, huwa hivi…
Wakati baba amekaa sebuleni usiku akiangalia
tivii ‘kiuongo’, yeye anaosha vyombo nje, tena si
ajabu amevitawanya kiasi kwamba, kama ni
kumaliza ataweza kwenda hasi usiku wa manane.
Na kila baada ya dakika tano, msichana huyo
ataingia ndani na kupita mbele ya baba. Lengo
lake ni kusoma mazingira kama mama mwenye
nyumba amelala.
Kwa vile wao si waanzaji (kama ilivyo tabia ya
mwanamke), basi unaweza kumwona
anashikashika vitu vya sebuleni, kama vile
kuweka sawa vitambaa vya makochi (japo ni
usiku), kufuta meza, kabati au wakati mwingine
kupanga CD za muziki au filamu ambazo zipo
kwenye shelfu lake. Mambo hayo anayafanya
huku vyombo vikimsubiri nje!
Hapo anachotaka, baba amuone kirahisi na
kuanza kumtekenya-tekenya, kumshika-shika
hatimaye ‘kumalizana’.
Utashangaa, ukifuatilia sana, utakuta hausigeli
akishamalizana na mume, vyombo anaviingiza
ndani na kuvimalizia kesho yake asubuhi.
Kwa maana hiyo pia, wake za watu wawe macho
na wasichana wa kazi wanaoshindwa kumaliza
kuosha vyombo usiku.
MAENEO YA UFUSKA
ni vyema niweke wazi maeneo ambayo ma-baba
wenye nyumba ndiyo hupenda kutumia kufanya
mapenzi na wasichana wa kazi.
Ni vigumu sana kukuta wawili hao wanamalizana
sebuleni (ingawa inawezekana sana) kwani ni
eneo hatari kuliko yote ndani ya nyumba.
Uchunguzi wa kina wa kimazingira umegundua
kuwa, kati ya maeneo hatari kwa fumanizi ndani
ya nyumba ni sebuleni.
Wengi waliowahi kufumaniwa, mfano mume kula
uroda na shemeji yake (mdogo wa mkewe) au
binti kuliwa uroda na hausiboi, ilikuwa sebuleni.
Aidha, sebuleni ndiyo mahali panapofikwa kwa
mara ya kwanza na watu waliolala ndani ya
nyumba kuliko sehemu nyingine yoyote.
Kwa hiyo, mababa wengi sasa hukwepa sebule
na kwenda chumbani kwa msichana, stoo,
bafuni, jikoni kama liko pembeni na uani, hasa
maeneo yenye vificho kama nyuma ya karo au
kama kuna sehemu kumesimamishwa vitu
chakavu.
Chooni si sana kwa sababu ni eneo linalofikwa na
watu kila wakati karibu usiku kucha.
Sasa hatari ipo hivi, mke asiyejua haya, kama
mumewe ataendelea kimapenzi na hausigeli,
hufikia wakati uhama nyumba. Namaanisha
kwamba, hufika mahali wakitaka kukutana
kimwili, wanakwenda gesti.
Gesti zao mara nyingi ni nyuma ya nyumba au
mtaa wa pili, huwa hawaendi mbali sana kwa
kuogopa muda wa msichana kufanya kazi za
ndani.