Sunday 22 June 2014

MAPENZI UTUNDU SIO UCHAWI JAMANI...JIFUN


LEO nimependa kuongelea kuhusu namna ya kudumisha penzi iwapo wewe umeolewa hasa kwa kina mama ambao penzi lao linaelekea kuyeyuka. Na bila jitihada za hapa na pale penzi lako na
mumeo linaweza kunyauka kabisa!!! Na ukumbuke wahenga walisema PENZI ni MAUA kuna
kuchanua na kunyauka. 
Na penzi linaponyauka huwa yanatokea maumivu makali sana ndani ya moyo, maumivu ambayo hayana kifani. Sasa ufanye nini ili penzi lako lisinyauke? Zingatia yafatayo: i) Hakikisha unakuwa karibu na mumeo
ii) Mumeo akirudi kutoka safarini au kazini umpokee kwa mabusu na upendo wa hali ya juu 
iii) Kama utakuwa na nafasi jitahidi kumuandikia msg mumeo za upendo na kumfariji 
iv) Na mwisho kumbuka kuwa mnapokuwa katika sita kwa sita jitahidi kutoa sauti ya mahaba huku ukijitahidi sana kumpa penzi kutumia ujanja wako, na kama atamaliza mwambie "POLE MUME WANGU"

Kwa leo ninakomea hapo kumbuka kuwa wanaume ni watu wa kujaliwa kila wakati na kubembelezwa Mwanasaikolojia wa mapenzi Dr. Linda wa chuo kikuu cha Oxford aliwahi kunena ya kwamba hakuna dawa ya mapenzi zaidi ya kuonyesha upendo kwa umpendae.