Wednesday 18 June 2014

JINSI WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA WANAUME ZAO

1: KAULIMiongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka
kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke
akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa
amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea
kupotea nguvu za kiume taratibu.Msaada unaohitajika kwa mwanamke
anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali

ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume
zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: "Yaani
siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!"2 : UJUZIWanawake
wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa.
Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume 'kuwika', si wabunifu na watundu,
jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa
hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo,
hawezi
kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.Pamoja na
wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye
sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo
huo.Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa 'kazi', lakini
pale wanapogeuzwa 'chekechea' hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu
hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu
wa nguvu za kiume.Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwana uelewa
mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango
kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na
maneno kama: "Leo nakuja kukupa vitu adimukuliko vya juzi, hakuna
kulala kasi mtindo mmoja." Kauli hizi huwaogopesha wanaume na
kuwafanya wapungukiwe na nguvu.3:USAFIMwanamke anapokuwa si msafi,
huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.
Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa
tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume
apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na
mwili ni muhimu sana katika mapenzi.4:GUBUJambo lingine linaloweza
kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za
maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala
miguu. Uchokonozi wa
mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo
yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.Mwanamke
anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya
mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha
kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe
na msisimkowa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao
hao.5:USALITITabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha
mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume
anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni,
maumivu ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo
humuondolea hamu ya tendo.
--
www.chinjithegreatson.blogspot.com