Monday 11 May 2015

KWA NINI WAPENZI WANACHOKANA HARAKA?

Kwanza niwashukuru wasomaji wangu wa safu hii walionitumia ujumbe mfupi wa maneno wakiipongeza mada hii.


Wiki iliyopita tuliishia kwenye kipengele cha pili cha Ujuzi faragha, leo tunaendelea na vipengele vilivyosalia, ungana nami.
KUTOTIMIA KWA MATARAJIO
Wapo wanaoanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu wakitegemea kufaidika kwa kitu flani, kama vile mabadiliko ya maisha yao na kadhalika, hivyo inapokuwa tofauti, hujiondoa mapema.
MAZOEA
Tatizo hili mara nyingi linawakuta akina dada. Wakishakuwa na mtu kwa muda mrefu huchukulia kuwa ni mazoea na hivyo kufanya wanavyotaka bila kujua kuwa wanawaudhi wenza wao, ambao ili kujiweka sawa kiakili huamua kusaliti na au kusababisha dharau baina yao.
KUTOJALI
Hii zaidi ipo kwa wanaume, pale mwanzo walikuwa wakijali kwa kusikiliza na kutimiza shida za wenza wao, lakini baada ya kupata walichohitaji, hawana tena ‘mzuka’. Jambo hili huwakera wenza wao na kujikuta wakiamua kukata mawasiliano mapema.Ushauri ni kwa wote, wake kwa waume, kila mmoja kuwa chachu ya ustawi wa penzi, badala ya kusubiri kufanyiwa unachotaka!
MAZINGIRA
Hii ni moja ya sababu ambayo pia inasababisha wapenzi wengi kuchokana haraka. Utakuta wapenzi wamezoea kukutana faragha chumbani tu hakuna hata siku moja ambayo wanabadilisha mazingira.
Wapenzi wanatakiwa kubadilisha mazingira kwani wasipofanya hivyo, hata akili huwa inachoka na hii haimaanishi labda muende hotelini, inawezekana hamna uwezo huo, basi fanyeni mabadiliko ya mazingira hukohuko nyumbani kwenu, yaani mnabadilisha maeneo, kama leo mlizungumza mkiwa sebuleni, basi kesho mfanye hivyo mkiwa kwenye kochi na siku nyingine mnaweza kushusha godoro chini!
MAWASILIANO
Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika mapenzi. Katika ulimwengu wa leo hakuna mapenzi kama hakuna mawasiliano.Hapa ninazungumzia wapenzi kuwasiliana kama kupigiana simu, kutumiana meseji za kuulizana umeshindaje, umekula, kazi na mengine mengi, hii ni kinga tosha ya kutochokana haraka, hivyo hata kama uko bize kiasi gani jitahidi kuwasiliana na umpendaye.
Wapo wapenzi ambao wanapitisha hata siku mbili au tatu bila kuwasiliana na wenza wao wakati mwanzoni mwa penzi lao haikuwa hivyo, walikuwa wanatumiana meseji au kupigiana simu kila wakati lakini siku zinavyokwenda ndivyo mawasiliano yanakuwa hafifu au unakuta mmoja yaani mwanamke au mwanaume ndiye anayejitoa kila wakati kujitahidi kuwasiliana na mwenzake, lakini mwisho anachoka na penzi linaishia hapo maana hakuna thamani au wanajikuta wanatafutana pale mmoja anapokuwa na uhitaji wa kimwili,