Thursday 7 May 2015

Mwanaume Akikuhudumia/Kukuweka Mjin Cha Moto Utakiona! Hela Yake Utaila Lakini Chamtemakuni Utakiona



Kuna bi dada tu nilikutana nae coz namfahamu BF wake. Huyo BF ni senior bachelor miaka kibao! Sasa ndo akatutambulisha kwa huyo dada kuwa mchumba wake na anataka kumuoa ASAP! Mmmmmmmmh! Tukasema haya. Basi masikini mdada wa watu msweet tu, akawa anaitaka kweli ndoa. Akawa anatuuliza nyie(Sisi) vipi mbona vidole vyeupe afu hatuna stress? Tukamwambia sie migumegume iliyomshinda mtume! Wala hata usihangaike na sisi, hapa kuna walioachika, waliozalia nyumbani, wasiojielewa yaaaaani we acha tu! Akawa anasema nyie wadogo ndo maana hamstuki! Tukamwambia sisi hatuna udogo wowote, hatujielewi tu. Bai akawa anatuambia kahangaika sana mpaka kumpata huyo Senior bachelor, atleast anasomeka! She was so desparate.!!!!! Sisitukamwambia good for you! Tunkutakia kila lililo la kheri. Wachangaji maarufu tupo.Siku ingine nimekutana nao na Senior bachelor akawa mnyongeee, mimi nika mind my own business! Mara niko chooni kaingia na kuachia ukunga na kilio cha nguvu! Mi kutoka na kumuuliza kulikoni! Akaniambia acha tu, kazidi kulia! mi nikambembeleza tu, sikuuliza sana. (Wapendnao wkigombana shika jembe ukalime wakipata vuta kapu ukavune). Basi ikawa kila nikimuona hana rahaaa! Mnyongeee! Siku nikaona ananaswa vibaokwenye gari ya senior bachelor! Nikasema uchumba huu! Balaaaaaaaa!Huyo mdada mzuri nyie acheni tu. Afu mkarimu ana roho nzuri, mcheshi! Nikasema kweli Senior bachelor kapata mke! Lakini why does she look very unhappy? Nikamuuliza siku. Ndo akaniambia yeye ana mtoto alizaaga kabla, anamlea mwenyewe! Sasa senior bachelor HAMPENDI yule mtoto kabisaa, kabisaaa. Na yeye hana kazi so anamyegemea Senior bachelor amuweke mjini. Sasa Senior Bachelor hatoi hela yoyote ya matumizi ya mtoto. Nikamwambia si utafute kazi? Akasema yeye hajasoma hivo kazi kupata ni shida sanaa! Nikamwambia sasa si usome saivi ushaona umuhimu wa shule? Akasema mambo mengi bwana, we acha tu. Maishayangu ndo basi tenaaa. Mi nikamwambia fm 4 atafute kozi tu aende. Bila kujikomboa kielimu atanyanyaswa kila aendako.Huku senior bachelor manyanyaso yakazidi mara mia! Hamna kitu kibaya kwamzazi kama mtu umpendae amchukie mwanao! Unashindwa kujigawa! Mara senior bachelor amwambie hajasoma mjinga! Yaani ilimradi basi tu! Baadae nikasikia kabwaga manyanga! Huyo kakisanua kwa seniorbachelor kavuta zake jibaba!Nikaja kukutana ane akaniambia nashukuru sana ule ushauri ulionipa ni wambolea sanaa. Nimesoma certificate, nangojea kuanza Diploma! Yaani nashukuru sana thamani yangu imeongezeka sanaaa, na nimejitambua!Nilitumika sanaa na wanaume ili nitoke lakini wapi. Nimepata na kazi namhudumia mwanangu, na nimepata Mchumba mwingine. Kweli bila elimu/ biashara hela ya mwanaume ina masharti kama ya mganga wa kienyeji! Haswaa akikuona huna kitu!MKURABITA! MKURABITA! MKURABITA! Jikomboe kiuchumi mwanamke mwenzangu, Kama ulikimbia umande, rudishule, makozi kibao, hujachelewa! Hata ukichuna lipia ada ama Fungua biashara na hio hela iwe mtaji sio kuitapanya kwa kuweka heshima town na kuishia kuaibika uzeeni! Hela ya kuchuna tamu lakini haidumu, na uzuri ni wa mda tu! Kuchuna iwe means to an end sio ndo the end!!!!!!!!!