Wednesday 6 May 2015

Nimependwa na mpenzi wa mtu naomba ushauri



Jamani nina rafiki yangu anaesoma katika college flan, kanipigia cm siku moja iliyopita anadai kuwa kwa sasa yeye ni binti anayeelekea mwaka wa pili pale chuoni na toka awe hapo ni almost wasichana wote walipata wapenzi isipokua yeye na hata walifikia hatua ya kumbeza na kumcheka kwa kumuona kama vile hayuko kamili. Si hivyo tu bali anahitaji sana mtu wa kuwa karibu nae(mpenzi) na anapenda sana mtu wa kumliwaza sexually,lakini kadri anavyozidi kupanda kimasomo ndio rate ya kufatwa na wanaume inapungua.sasa hivi kuna mkaka mmoja ambae tayari ana mpenzi wake pale chuoni amemtongoza na anadai anamueleza maneno matamu ambayo sio siri yanamteka.Japo anajua ni mpenzi wa classmate wake lakini pia yeyeamevutiwa nae na ukiongezea hali yake yaukata wa kimapenzi ndo basi kabisa haonijibu la NO.sasa anauliza afanyaje? na je labda itakuwa ni risk? lakini bado anasisitiza kwa hali yake hiyo pia akimkataa si ataendelea kupata tabu? ushauri jamani!