Thursday 14 May 2015

HIZI NDIZO SABABU ZA WANAWAKE WENGI KUCHELEWA KUOLEWA NA KUISHIA KUSAGANA TU

Pamoja na kuwa kuna wanawake husita 
kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana 
kwa wanawake kama ilivyo kwa 
wanaume. 
Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka 
kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi 
ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo 
kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana 
na shamra shamra awazo nazo mwanamke 
wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa 
na Harusi. 
Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache 
ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya 
sababu zinazopelekea kusuasua huko. 
(Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao 
hawajawahi kuolewa kabisa) 
Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa 
muonekano) 
Wanawake wengi hasa wa umri mdogo 
(lakini unatosha kuolewa) hutumia muda 
mwingi katika kuchagua aina ya 
mwanaume ambaye angependa awe 
mume wake.Wanawake hawa hujiamini 
zaidi na kusimamia sifa zile ambazo 
huamini ni muhimu mwanaume wa 
kumuoa awe nazo. 
Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya 
muonekano wa mwanaume huyo – kuna 
wale ambao hutaka mwanaume huyo wa 
kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, 
aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri n.k. 
Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana 
ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna 
wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa 
ila hataki sababu tu huyo mwanaume 
hafananii vile ambavyo yeye anataka 
mumewe awe. 
Kutaka mwanaume tajiri 
Kuna wanawake ambao tayari 
wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali 
kuolewa na mwanaume yeyote yule 
ambaye hana pesa nyingi. 
Yupo tayari kuolewa ila si kwa mwanaume 
mwenye uwezo wa kawaida – hata 
ikitokea mwanaume ana uwezo kidogo wa 
kuweza kujitosheleza, yeye bado huona 
huyo mwanaume hamfai hadi pale tu 
atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi 
maisha ya kifahari. 
Hivyo hukazana kusubiri na kujitahidi 
kuwinda aina ya mwanaume ambaye 
atakuwa na uwezo mkubwa, bila kujalisha 
kama huyo mwanaume kampita sana umri. 
Kutompata Mwanaume Ampendae 
Hili ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume 
ambao huamini ndoa haiwezekani na 
haifai bali tu hadi pale umpatapo yule 
ambaye unampenda na unaamini 
anakupenda pia. 
Wengi katika kundi hili huamini kuwa 
mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni 
kupendana tu na mengine hufuata kwenye 
sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo 
vya mwanamme awe vipi havina umuhimu 
kabisa katika kutaka kuamua kuolewa. 
Yeye kikubwa anataka ampate mume 
ambaye atampenda kwa dhati na huku 
akiwa na matumaini kuwa huyo mume 
atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu 
mwanamke anaamini msingi bora wa ndoa 
ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe 
basi! Hana haraka hadi pale atakapompata 
mwanaume akampenda ndipo 
atakapokuwa tayari kuolewa. 
Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa (SO 
SELECTIVE) 
Kuna wale wachache ambao akili 
hubadilika kama kinyonga; wasioridhika 
wala kujitambua ni nini wanataka ama 
mwanaume wa aina ipi wanataka. 
Akija wa mwenye uwezo atasema nataka 
wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo 
atatoa sababu tu hata kama kumlaumu 
kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta 
maendeleo. 
Akija wa kabila hii, atasema hapana hao 
wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi 
ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale 
ambao wanajitokeza kutaka kumuoa. 
Hatimaye inaweza tokea muda wa kuolewa 
ukapita na akaishia kupunguza 
uchunguzaji lakini ikiwa hata wanaume wa 
umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena 
katika soko. 
Kujiona ni mzuri sana 
Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi 
Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa 
muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi 
kwamba wake kwa waume wote 
wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote 
kumtamani. 
Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao 
huwa ni wazuri kawaida – ila kwa 
mtazamowake hujiona ni mzuri mno 
hakuna mfano kama yeye; kitendo 
ambacho kwa wachache kwenye kundi hili 
hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa 
yeyote kuwa na yeye huyo mtu anatakiwa 
atambue kuwa ana bahati sana. 
Kitendo hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya 
mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi 
kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka 
kuoa – anaweza onyesha tabia kama 
maringo, dharau na kiburi. 
kujiona ana Umri mdogo 
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea 
anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia 
kuolewa. 
Wanawake wametofautiana mipangilio yao 
ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri 
wa kuolewa hutamani sana kuolewa na 
kuna wale ambao hupenda kuolewa 
wakiwa wakubwa zaidi. 
Katika kundi hili umri kuwa mdogo 
hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na 
umri wa miaka 25 na bado akajiona 
mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na 
miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa 
kuolewa. 
Hii pia ni kwa wanawake wale ambao 
huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha 
katika ndoa. 
Anapokuwa na umri ambao anaweza 
kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa 
muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia 
katika ndoa. 
Maradhi hasa UKIMWI 
Hili kama lilivyo kwa wanaume - Pamoja na 
kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa 
maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa 
umeathirika unaweza kuwa na mahusiano 
na hata kuoa na kuwa na watoto; bado 
haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua 
kuwa ni waathirika wakiwa bado ni 
wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi 
kuwa na mtoto. 
Wengi sana hukata tamaa na huona ni 
kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika 
ndoa, hasa tokana na imani kuwa 
wanawake wakizaa wakati ni waathirika; 
afya hudhoofika zaidi. 
Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi 
kwa furaha milele) 
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia 
nyingi ambazo huonyesha maisha ya 
kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana 
kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo 
maisha ya tamthilia yawe na kwao pia. 
Hilo linafanya vigezo ambavyo mwanamke 
huyo anatumia kuchagua ama kukubali 
mwanaume kumuoa kutotimiza yale 
ambayo yeye binafsi anatarajia. 
Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna 
maisha ya furaha milele, na hasa kuwa 
maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya 
na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi 
kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo. 
Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa 
Mtazamo huu kwa wanawake wenye 
msimamo huu, huchangiwa na baadhi 
kama haya: 
- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea 
kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya 
ndoa, haki, majukumu na mengine mengi. 
- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza 
kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe 
(pengine mama aliteswa sana), na hata 
ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila 
ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke 
huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha 
ya taabu na kuonewa. 
- Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza 
ambao unaweza kumtimizia na kufanya 
lolote lile ambalo anataka katika maisha. 
Kwake kuwa na mwanaume kama mume 
kwake anaona kama ni utumwa. 
Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za 
kufanya mapenzi 
Kuna wanawake wale wachache 
waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile 
ya kimwili ya kuweza kupata hisia za 
kuweza kujisikia ama kutamani kufanya 
mapenzi. 
Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni 
waoga sana wa kuwa karibu na 
mwanaume, na kwa wale ambao 
wamewahi hata jaribu baadhi huona kama 
kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na 
uchafu. 
Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia 
kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara 
kinamvunja kabisa hamu ya kutaka 
kuolewa.