Saturday 9 May 2015

HATARI SANA! AMINI USIAMINI, UZEMBE HUU UTAKUPOTEZEA MUMEO KWAHAUSIGELI WAKO!

Mfumo wa maisha ya familia nyingi 
siku hizi unawalazimu wahusika kutafuta 
wafanyakazi wa ndani (mahausigeli) kwa 
ajili ya kuwasaidia kazi. Ni uamuzi mzuri 
kwa sababu hurahisishakazi ya kutunza 
familia na wengi huwa msaada mkubwa, 
achilia mbali wale wachache wenye tabia 
zisizofaa. Hata hivyo, kadiri siku zinavyozidi 
kusonga mbele, vilio vya wanawake 
waliopo kwenye ndoa kulalamika kuibiwa 
waume zao na wasichana wa kazi vinazidi 
kuongezeka. Katika kila wanawake kumi 
wanaoishi na wasichana wa kazi, saba 
waliwahi kutendwa kwa waume zao 
kusaliti ndoa na mahausigeli au kujaribu 
kuwashawishi wavunje nao amri ya sita. 
Wanawake wengi ambao wapo katika 
uhusiano rasmi watakuwa mashahidi 
wahili. Yaani unaenda kumchukua dada wa 
kukusaidia kazi za nyumbani kijijini, 
unamleta mjini, unamhudumia kwa kila 
kitu, anaanza kuoga na kupendeza na 
mwisho unajikuta ukisaidiwa hata yale 
ambayo hukuomba kusaidiwa au ambayo 
hayastahili kuwa na msaidizi. Wanawake 
wengine wanajeruhiwa zaidi baada ya 
waume zao kuishia kuwapa mahausigeli 
ujauzito au kuzaa nao! Dada wa kazi 
anageuka na kuwa mke mwenzio. Zipo 
sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili na 
ningependa tuzijadili kwa pamoja.1. 
KUJISAHAUWanawake wengi wana kawaida 
ya kujisahau wanapopata wasichana wa 
kuwasaidia kazi. Kama kipindi cha nyuma 
kabla hajapata hausigeli mwanamke 
alikuwa akimfulia mumewe, kumuandalia 
chakula kizuri na kutunza vizuri familia, 
akishapata dada wa kazi, hujisahau na 
kuacha kutimiza wajibu wake kama mke. 
Matokeo yake, unakuta dada wa kazi ndiyo 
anashughulikia mambo yote muhimu 
yanayomhusu mume kuanzia anapoamka 
asubuhi mpaka usiku. Ndiyo! Mumeo 
akiamka asubuhi, dada wa kazi ndiyo 
anaenda kutandika kitanda, anamuandalia 
maji ya kuoga, anamuandalia kifungua 
kinywana kumnyooshea nguo za kuvaa 
siku hiyo. Mchana au jioni akirudi, yeye 
ndiyo anampokea, anamuandalia maji ya 
kuoga kisha anamuandalia chakula cha 
usiku. Yeye ndiye anayefua nguo zote za 
mumeo, hata zile ambazo hastahili kuzifua. 
Unategemea katika mazingira kama haya 
nini kitatokea kama siyo mumeo kuanza 
kumpenda hausigeli? 2. UKARIBU 
ULIOPITILIZASuala lingine ambalo 
linawaponza wanawake wengi waliopo 
kwenye ndoa, ni kuruhusu waume zao 
wawe naukaribu wa kupitiliza na 
mahausigeli. Kutokana na ubize wa kazi au 
mtindo wa maisha, unakuta mwanamke 
anakuwa bize na mambo yake mengine na 
kusahau wajibu wake wa msingi wa kuwa 
karibu na mumewe. Kwa mfano, usiku 
mama anawahi kwenda kulala kwa 
kisingizio cha uchovu na kumuacha 
mumewe na hausigeli wanatazama 
runingapamoja sebuleni. Au unakuta 
asubuhi, mama wa familia anawahi 
kuondoka kabla ya mumewe na kuacha 
mwanya wa wawili hawa kuwa karibu na 
kuzoeana. Jioni pia, baba anawahi kurudi 
nyumbani lakini akifika, mkeweanakuwa 
bado hajarudi au hata kama amerudi, yuko 
bize na mambo mengine kabisa. Hakuna 
mtu anayependa kukaa na upweke kwa 
hiyo kwa sababu umeshindwa kutimiza 
majukumu yako, taratibu atahamishia 
ukaribu kwa dada wa kazi, watazoeanana 
kuanza kuvukiana mipaka. Unategemea 
mwisho utakuwa ni nini?Tukutane wiki 
ijayo kuangalia ni mambo gani unayopaswa 
kuyafanya ili kuondoa kabisa mianya ya 
kuibiwa mumeo na hausigeli wako. Kwa 
maoni, ushauri, tupia comment hapo chini.