Monday 18 May 2015

Je, unajua mwenza wako anakupendea kitu gani?



MARA nyingi kosa la kutohangaika kujua wenza wetuwamevutiwa na vitu gani kuhusu sisi, huwa ni kubwa na mwisho wake siku zote huwa majuto ni mjukuu.Wengi wetu hujiingiza kwenye uhusiano kichwa kichwa hasa baada ya kutawaliwa na mapenzi, hali ambayo humfanya mtu awe kipofu hata katika mambo ambayo yanaonekana na yanayoweza kuzuilika.Katika uhusiano ni muhimu kujiuliza pale mwenza wako anapokuambia anakupenda, jaribu kudadisi ni vitu gani ambavyo vimemvutia kwako.Je, ni muonekano wako, sura yako, tabia yako, umuhimu wako katika jamii, fedha zako auucheshi wako ni muhimu kuzifahamu hisia za mwenza wako huyo juu yako ili uweze kujua ni aina gani ya uhusiano ulio nao.Kwa kufanya hivyo ni wazi kuwautagundua msimamo wa uhusiano ulionao kwani iwapo mwenza wako atakuwa anakupendea muonekano wakona sura yako na tabia yako na mambo ambayo si rahisi kubadilika basi kuna matumaini katika uhusiano huo.Lakini iwapo utagundua kuwa anakupendea jina lako, uwezo wako kifedha na vitu ambavyo vinaweza kubadilika katika maisha ni vyema umuepuke mwenza kama huyo kwani mambo yakigeuka hapo baadae,kuna hatari ya kukuacha na kuumiza moyo wako.Ni vyema kutambua kuwa kama penzi na uhusiano wako umejengwa katika msingi wa fedha ama jina ulilonalo, vitu hivyo mara nyingi katika maishahubadilika hebu jiulize mwenyewe je, umaarufu wako utakapopungua ama fedha zikikuishia uhusiano huo utakuwa wapi?Jibu liko wazi mwenza wa aina hiyo si mwenza na wala hakutakii mema, yupo nawe kwa kutimiza matakwa yake na pindi atakapomalizika anachokitaka atakuacha solemba.Lakini pia utakapogundua kuwa mwenza wako anakupenda kutokana na kuvutiwa na wewe kama wewe, sura yako, muonekano wako, tabia yako naucheshi wako vitu ambavyo unauhakika hata miaka mingi ijayo si rahisi kubadilika, basi uhakikawa penzi lako ni mkubwa zaidi.Hivyo basi, jambo la muhimu ni kuwa na uhakika na wenza wetupindi tunapotaka kuanzisha uhusiano, hiyo yote ni katika kulinda hisia na mioyo yetu katika suala zima la mapenzi.Wapo watu ambao wanajutia uamuzi wao kwa kutokuwa na nafasi ya kuchunguza hisia za wenza wao na kukimbilia kuwa na uhusiano, matokeo yake zile sifa zilizowavutiwa wenza wao zilipokwisha ndio ulikuwa mwisho wa uhusiano wao.Tuamke sasa hakuna ubaya katika kumchunguza kwanza mwenza hata kama unampendavipi, ni vyema kujihakikishia kwani hata kama kivuti ni fedha zako iko siku utaishiwa hapo ndipo utakapojuta, waswahili wanasema, heri nusu shari kuliko shari kamili.