Saturday 9 May 2015

JEUNALITAMBUA HILI KUWA WANAUME MASIKINI NA WASIOJIAMINI WANAONGOZA KUTONGOZA KWA MESEJI NYINGI HALAFU NDEFU ZAMA HAPA


Nimekaa sehemu leo napata lunch, mara 
dada mmoja mrembo aliyekuwa karibu 
yangu "kareact", "mameseji kibao halafu 
marefu, hayaeleweki. 
Unanijazia tu inbox, utakuwa masikini tu 
wewe halafu hujiamini".Dah, nilishtuka 
sana. Baada ya dakika kama 2 hivi.. 
nikamuuliza dada yangu mbona hasira 
sana, kwa nini. 
Akanijibu "kuna jianaume linanijazia tu 
inbox, linatuma messages nyingi, ndefu 
halafu halieleweki, wiki ya pili sasa, mie 
ananiudhi!" 
Nikamwuuliza "mbona unasema atakuwa 
masikini,akajibu "mtu mwenye hela zake 
na anayejiamini atahangaika kutuma 
mameseji kibao, marefu ambayo hata 
hayaeleweki." 
Kwani huyo hawezi kuwa tajiri, lakini 
kumbe anafanya ufafanuzi kwa kuandika 
kwa kina,"ingawa simjui, atakuwa hana 
lolote, anafikiri akijieleza au kuandika sana 
nitamhurumia au nitamwelewa, akafie 
mbele huko, tena namblock, hii ni kawaida 
ya wanaume kapuku."