Saturday 16 May 2015

HIZI NDO NJIA MUHIMU ZA KUMSHAWISHI MPENZI WAKO KAMA HAKUBALI KUTOA PENZI



Mmh! Haya sina jinsi kwa vile nimeamua kusema acha niseme, japo waswahili wanasema pilipili usiyoilamba hujui kuwasha kwake. Lakini mtwanga pilipili hakutaarifu ukohoe, hilo likae akilini. Leo jamani kidogo nimeingia kwenye mavazi, najua mmeanza kunitazama kina dada wapendao kutembea uchi.Kwa kweli ifike hatua ujionee aibu kabla hujakosolewa na walimwengu, unavaa nguo kama mkia wa mbuzi, haistiri mwili wala haikupendezi. Hivi jamani huoni raha pale mpenziwako anapokupapatikia baada ya kuondoa nguo mwilini kwani alikuwa akiutamani ukiwa ndani ya nguo, vikiwa mezani hamu inaongezeka mara dufu.Mwanzo nilidhani ni sisi wakina sina mume ndiyo huvaa mavazi ya mitego ili angalau tukikosa papa basi tupate dagaa mchele. Lakini kumbe sivyo, wengine wake zawatu na mumewe anatazama kesho ukisikia katembea na mkata majani unakuja juu. Nani alikuambia mbuzi anajichunga mwenyewe.Huu utandawazi umewafanya wanaume wengi kuwa mazezeta, jamani wazazi wetu ndivyo walivyotulea? Mtoto wakike enzi zetu ulikuwa huoni matiti wala mapaja, nguo ya ndani ndiyo usiseme, shangaamamaaaa utazionea wapi.Ilikuwa aibu kubwa kwa mtoto wa kike kuonesha vitu hivyo, lakini leo mwanamke kageuka mbuzi, kutembea uchi wala hajali. Watoto wa kike tokea ndani ya nyumba zao wanakaauchi eti kwenda na wakati. Jamani tunakwenda wapi mbona tunapotea?Sasa hivi wasichana wanavaa nguo fupi nguo za ndani nje shanga ndiyo usiseme. Sasa hivi changudoa hajulikani na mke wa mtu vilevile, wote mwendo huohuo. Mnajua nini hili nalisema bila hofu sikuogopi japo litakukera. Sisi wanawake tuna akili za kushikiwa kila kitokacho lazima tukifanye, ukija mtindo wa kuvaa magunia wote tunavaa ili mradi tusipitwe na wakati.Kwa vile hatutaki kupitwa na vitu hata wanawake walio ndani ya ndoa wanaona machangudoa au wakosa haya kutembea uchi wanakwenda na wakati nao wanayafanya hayo. Aiii jamani,nataka kuwaeleza kitu kimoja ndoa ni zaidi ya kupiga goti kwenye madhabahu.Mungu anaitambua ndoa, ndiyo maana huwakusanya watu kuishuhudia wakiwepo viongozi wa dini. Tukiambiwa tuna akili ya mbuzi tusikasirike.Jamani tuheshimumavazi, utu wetu matendo huonekana kwa macho ya moyoni ni siri ya mtu. Huwezi kusema tabia yangu nzuri wakati unatembea uchi.Tujistiri basi, ili tudumishe heshima ya mwanadamu, tujitofautishe na wanyama.Sasa hivi tumekuwa wanyama, kutembea uchi na kufanya mambo ya aibu bila kuona haya.Hata kuaga nimesahau mnaniudhi ati, tukutane wiki ijayo. Anti yenu Nasra Shangingi Mstaafu.