Wednesday 13 May 2015

SHTUKA! ZIJUE SABABU ZAWANAUME KUCHEPUKA!


Mambo vipi msomaji wa safu hii. Bila shaka unaendelea vizurina harakati zako za kimapenzi na kwa mara nyingine upo tena katika safu hii ili kufuatilia nini kimejiri.Moja ya tatizo kubwa kabisa linalowasumbua wapenzi wengini tabia ya kutoaminiana baina yao. Kila mmoja hudhani mwenzake anakwenda kinyumena hili, mara nyingi lawama huenda zaidi kwa wanaume kwani ni wepesi kuchepuka.Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazosababisha wanaume kutoka nje ya uhusiano wao wa kimapenzi. 1. Hulka(Tabia)Wanaume wengine wana tabia tu ya kupenda kuwa na wapenziwengi, hawaridhiki na mwanamke mmoja. Hawana hofu ya Mungu na hili hulifanya hata kama hakuna ugomvi wowote nyumbani. Kwao, kile demu aliyependeza anayekatizambele yao wanamtamani.2. Kutojiachia faraghaLabda hili wengi hawapendi kuliweka wazi. Wanawake ni watu wa aibu, hawapendi kujiachia kwa kuonesha wanachojua chumbani, wanaamini kwa kufanya hivyo wataonekana wahuni. Kwa sababu hiyo hupenda kushiriki tendo ‘kistaarabu’ na heshima, tena hivyo hivyo kila siku, inachosha. Mwanaume anaona bora ‘akatesti’ ladha nyingine nje.3. Mkumbo Wanaume wengi hasa hawa vijana wa sasa wanafuata mkumbo wa marafiki kwa kutaka kufanana nao. Wakiona kila kwenye tukio flani wenzao wamekuja na ‘vitu vipya’ nao hutamani kuwa hivyo, hivyo kujikuta wakichepuka. Baadhi yao hujisifu kijinga kuwa hata wazazi wao walikuwa viwembe hivyo wamerithi.4. UmaarufuBaadhi ya wanaume hudhani kuwa kuchepuka ni sifa inayowapa umaarufu kwa kuonekana wao ni hodari. Wengine hutaka kuonesha kuwa wao ni vidume vya mbegu. Ingawa kimsingi inawaondolea heshima kwa kutongoza kila mwanamke anayekuwa mbele yao, lakini kwao ni fahari ya kujitapa nayo mbele ya wenzake. 5. MazingiraWakati mwingine wanaume huponzwa na mazingira wanayoishi au anayokuwemo. Akienda safari, kwa mfano aina ya marafiki na matendo yao wanapokuwa baa au sehemu yastarehe yanaweza kumgeuza juu ya mwenendo wake, hasa kwa wanawake. Huogopa kuonekana ‘mshamba’.