Monday 18 May 2015

SHTUKA! Fahamu Mbinu za kutofautisha rafiki na mpenzi!



SUALA la kushindwa kutofautisha rafiki uliyenaye kama ni rafiki tu na mpenzi wa kweli, ni la kawaida sana katika jamii na mara nyingi huwapata zaidi wanawake.Wengi wao hushindwa kutambua mwanamume ambaye anaweza kuwa mpenzi au rafiki na mwishowe hujikuta wakitumbukia kwenye uhusianoambao haufai kuwa uhusiano wa mapenzi.Sehemu yenye shida ni kutambua yupi ana nia ya kuwa na uhusiano wa mapenzi wa kudumu na yupi anataka kuwa rafiki, kwani kati ya wanaume wengi wanaokutana na mwanamke, lazima mmoja atakuwa na nia njema ya kuwa na uhusiano na mwanamke huyo. Sasa basi utamtambuaje?Je, kuna alama yoyote ya kukuonesha mwanamume kama huyo?Kwani inawezekana kabisa wanaume wengine pamoja na kuwa na nia hiyo, hawajui namna ya kuanza kuzungumzia suala hilo. Ukweli ni kwamba ili umtambue mwanamume anayekupenda na yule anayetaka urafiki wa kawaida tukwako, ni lazima utambue kwa kuzingatia sifa zifuatazo.Marafiki siku zote wana tabia yakuzungumza kwa uhuru zaidi, hutaniana na kucheka na mara zote huzungumza pamoja katika mtindo wa kuzoeana zaidi bila kuoneana haya.Kwa mujibu wa wataalamu na wachambuzi wa masuala ya mapenzi, kama mwanamume ana nia ya mapenzi na mwanamke, si rahisi kufanya mambo kama hayo.Acha tu kuongea kwa uhuru, itamuwia vigumu pia kuzungumza na mwanamke anayempenda na wakati mwingine unaweza kumkamata akimuangalia mwanamke huyo mara kwa mara, tena kwa macho yaliyo makini lakini maratu mwanamke huyo atakapomuangalia, ataangalia pembeni haraka.Kwa mwanamume mwenye hisia za mapenzi kwa mwanamke, si rahisi kumuangalia mwanamke huyo kwa uhuru na mara nyingi hufanya jambo hilo kwa kificho na hata katika kikundi, utaona watu wengine wanaongea na kucheka lakini yeye atatulia.Pamoja na ishara hizo atakazoonesha mwanamume huyo, pia kwa mwanamke anayependwa, ikiwa kwa bahati mbaya akajigonga kwenye kitu au kujikwaa, wanaume wengine waliopo wanaweza wasishituke,lakini yeye atainuka kwenda kutoa msaada. Kumbukeni kwamba kuwa na mtu mwenye hisia za mapenzi na rafiki kuna tofauti kubwa.Rafiki ni tofauti na mpenzi kwa kuwa hakuna nafasi ya mahaba katika urafiki na marafiki hushirikiana kila kitu bila kujali kulindana.Marafiki pia hawajali, hata wakiwaonesha rafiki zao upande wa pili wa tabia zao na mara zote hupenda kujionesha na kushirikiana kwenye hata mambo yasiyo na maana bila kujali tofauti na watu walio kwenye mapenzi.Ishara nyingine kuwa mwanamume uliyenaye hana nia wala hisia za mapenzi kwako, ni pale atakapokuwa akizungumza na wewe na mavazi yake au muonekano wake kwako kwa ujumla.Namna ya kuzungumza na mavazi vinaweza kukusaidia kutambua aina ya mtu uliyenaye, kwani mara nyingi marafiki huzungumza kwa kujiamini na kwa sauti bila kuona aibu au kujali mtazamo wako.Pia hata muonekano wa rafiki yako mbele yako, awe mwanamume au mwanamke haijalishi kwako, lakini si kwa mpenzi wake lazima atafanya mambo hayo mawili kwa makinikwa kuwa anajali hisia na mtazamo wa mwenza wake.Katika mtazamo wa hisia za mapenzi, mambo yote huwa tofauti kwani hauwezi hata siku moja kumkuta mwanamume au mwanamke aliye mapenzini akiwa amevaa nguo ambazo zitamfanya aonekane kituko mbele za watu.Watu wa aina hiyo siku zote hufanya mambo yao kwa lengo moja tu ambalo ni la msingi na maana kwao nalo ni kumfurahisha mwenza au mtu ambaye wanampenda.Halikadhalika si rahisi kumkuta mwanamume au mwanamke aliye katika hisia za mapenzi, akizungumza na mtu huyo anayempenda kama marafiki wanavyofanya, si rahisi kabisa jambo hilo kutokea.Siku zote watu wa aina hiyo si wawazi na huwa na tabia ya aibu hasa wanapomuona mtu wanayempenda kwani kitendo cha kuwa naye karibu tu, huwafanya wasiwe huru kabisa.Kwa mtazamo huu sasa natumaini mmefahamu tofauti kati ya mwanamume rafiki na anayekupenda, ni jukumu lenu wanawake kuchunguza kama mwenza uliyenaye anakupenda au anakufanya kifaa cha mapenzi.-via habarileo