Wednesday 13 May 2015

YAFAHAMU MADHARA SABA MAKUU YA KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE.


Kufanya ngono kinyume cha maumbile ni nini?Hii ni aina ya ngono ambayo mwanamke au mwanaume anaingiziwa uume mkunduni {samahani kwa ukali wa hili jina]…Tangu kuanza kwa karne ya 21 swala la kuingiliana kinyume na maumbile limekua la kawaida sana hata kwa wapenzi wa kawaida yaani msichana na mvulana, japokua zamani kidogo ilikua ni kwa mashoga tu.Tabia hii Imesababishwa hasa na video za ngono za nje ambazo nyingi huonesha ngono hii kama ni ya kawaida na wala haina maumivu lakini ukweli ni kwamba hii sio ngono ya kawaida na huambatana namaumivu makali....utafiti uliofanyika uingereza imegundulika zaidi ya asilimia thelathini ya wapenzi wa kawaida wanashiriki aina hii ya ngono.Lakini pia kumekua na hadithi za uongo hapa nchini kwamba mwanamke akishiriki aina hii ya ngono basianaongezeka makalio kitu ambacho sio kweli kabisa.Leo ntaongelea madhara makuu ya kushiriki aina hii ya ngono..Kulegea kwa misuli ya mkundu;mkundu una misuli maalumu ambayo hubana kinyesi kisitoke wakati umebanwa mpaka utakapofika chooni, lakini tabia hiihulegeza sana misuli hii na kushindwa kujizuia pale unapokua umebanwa na kuweza kuadhirika wakati mwingine.Kansa ya mkundu; virusi maarufu kwa jina la humanpapilloma virus wanaopatikana kwenye eneo la mlango wa uzazi huweza kuambukizwa na kwenda kwenye mkundu na kusababisha kansa ya mkundu. Mashoga wengi wana hatari ya kupata kansa hii mara kumi zaidi ya wanaume wa kawaida.Maambukizi ya virusi vya ukimwi: mkundu hauna maji ya kulainisha njia wakati wa kufanya ngono hivyo hatari ya maambukizi ya ukimwi ni mara kumi zaidi kuliko mtu anayefanya ngono ya ukeni, hivyo kuendelea kushiriki ni kuendelea kujihatarisha.Magonjwa ya njia ya mkojo:tabia ya kuhamisha uume kutoka kwenye mkundu kwenda kwenye uke husambaza bakteria ambao huweza kupita kwenye tundu la mkojo na kushambulia kibofu cha mkojo na figo.Magonjwa ya zinaa; kama zilivyokua aina za ngono zingine, aina hii huambatana na magonjwa kama kaswende, gonorhoea, na mengine mengi..Fistula: vidonda visivyouma {ulcers} ambavyo husababishwa na tabia hii huweza kuleta tundu kati ya uke na mkundu au uke na kibofu cha mkojo, hali ambayo husababisha choo kubwa kutokea kwenye njia ya uke na mkojo kutoka bila kuzuilika.Hemorrhoids:hii ni mishipa ya damu inayovimba mkunduni na kuleta shida wakati wa kujisaidia haja kubwa, huweza kutibiwa na dawa lakini upasuaji huhitajika kama dawa zikishindwa{hemorrhoidoctomy}