Saturday 9 May 2015

TAMBUA JINSI YA KUONGEZA MVUTO KWA MPENZI WAKO

Kama umeshushwa thamani unakuwa 
kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama 
mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la 
kuingia kwenye ndoa na wewe lakini 
kwa sababu ameshakushusha thamani 
ndoa inaweza kuyeyuka. 
Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi 
maana mwenzako hukuchukulia wa 
kawaida – mazoea huzidi na hapo ndipo 
uhitaji wa kuwa na mwingine wa 
pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu 
tena kwako, ndiyo maana wazo hilo 
huvamia ubongo wake kwa kasi sana. 
Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, 
mwenzako atagoma kuongozana na 
wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana 
na rafiki zake njiani hatakutambulisha. 
Hisia kwamba hamuendani humwingia. 
UNAFANYAJE SASA? 
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki 
yangu mpendwa, suala la kupanda au 
kushuka thamani lipo mikononi mwako. 
Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, 
mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia 
hatua ya kukushusha thamani. 
Tayari tumeshaona athari zake lakini 
hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo 
ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi 
kwako kubaki namba moja na mtu 
muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) 
kwa mpenzi wako maana ni haki yako. 
ANZIA MWANZO 
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako 
kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. 
Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo 
hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi 
zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti 
kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni 
mambo gani hayo? Twende hapo chini. 
CHUNGA KAULI ZAKO 
Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni 
maalum zaidi kwa wanawake. Kitu 
muhimu cha kwanza kabisa kwa 
mwanamke ambaye anataka kuilinda 
thamani yake kwa mpenziwe ni kupima 
sana kauli zake. 
Acha kuropoka hovyo, pima maneno 
yako na ikiwezekana kama unadhani 
kuna jambo huna uhakika nalo 
usizungumze kabisa. Katika eneo hili, 
uwe makini zaidi mnapokuwa na watu 
wengine. Kama mwanamke usiwe 
mchangiaji hoja sana. 
Utulivu wako unaweza kuwa silaha 
kubwa ya kukufanya ubaki na thamani 
yako kama mwanamke anayejitambua. 
USIRUHUSU MAPENZI 
Msichana mwenye kujitambua na 
kufahamu thamani yake sawasawa 
hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane 
na mwanaume harakaharaka. Onesha 
unajitambua na usikubali kirahisi 
kuuacha mwili wako uchezewe. 
Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa 
wala kukuchumbia, haraka ya nini? 
Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi 
lako, lazima ufikirie kuhusu athari 
zinazoweza kukupata kwa kukurupukia 
mapenzi. Mwanaume ambaye bado 
hamjachunguzana na huna uhakika naye 
wa kutengeneza maisha, kichwani 
mwake hakuweki kwa asilimia kubwa. 
Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo 
yoyote – binafsi au yanayosababishwa na 
uhusiano wenu, anakuwa hana 
uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo 
hilo. Utabaki wewe na matatizo yako! 
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo 
ya Mapenzi, ameandika Vitabu vya True 
Love, Let's Talk About Love na All About 
Love vilivyopo mitaani. 
Chanzo: Global Publisher