Wednesday 2 July 2014

Na utundu Wangu Wote MAPENZI Yamenipiga Teke Mie!

Pole kwa kazi nzito ya kutwa nzima ya leo. Naitwa hilda nina miaka 24 nilijiingiza kwenye mahusiano namvulana mmoja ambaye nampenda sana tulikua tunasoma wote chuo kimoja baada ya kumaliza chuo kila mmoja akaenda
kwao tuliagana vizuri, akaniahidi kuwa baba wa wanangu baada ya muda. Kila mmoja akiwa kwao mawasiliano yakawa yamepungua nikawa namlalamikia sana juu ya yeye kutokunitafuta.

 Rafiki nisikufiche huyu mvulana nampenda sana hili lilinipelekea kuwa na wivu sana juu yake nikahisi naibiwa kwa sababu tulipokua wote chuo alipenda kuniambia ananipend sana ila baada ya kuagana hakuwa ananiambia tena. Siku moja nikamuuliza kwa nini hanitamkii tena kama ananipenda hakunipa jibu la moja kwa
moja nakumbuka hiyo siku nilimlalamikia sana.

Siku moja akanitumia sms akaniambia amechoka kulaumiwa hataki tena uhusiano nililia nikajaribu kumplease akakataa akasema anataka tuwe marafiki tu.
Kiukweli nampenda sana natamani arudishe moyo wake kwani ni yeye wa pekee katika moyo wang.