.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’,
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Chiki alisema kuwa yeye na Ray hawakuwahi kuwa na bifu kama inavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii isipokuwa walipishana kauli kidogo katika bethidei ya muigizaji Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ iliyofanyika
katika Hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar lakini waliyamaliza.“Sina bifu na Ray tuko poa, pale Lamada tulipishana maneno kidogo tu ila kwa sasa stori kama kawa hatuna bifu la aina yoyote,” alisema Chiki.
Kwenye bethidei hiyo, ilidaiwa kuwa Chiki aliyekuwa MC wa shughuli hiyo alimpa maneno ya ‘madongo’ kumsisitiza atoe mkwanja ‘fedha’ nyingi kama zawadi kwa Dk. Cheni hali ambayo ilimuudhi Ray.
Imeandikwa na Maria Halimoja na Rhoda Josiah.