Thursday 31 July 2014

AIBU MKE WA MTU AZIANIKA PICHA ZAKE ZA OVYO KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK...NI AIBU KUZIONA INASIKITISHA

Ama kwa hakika hivi sasa dunia ni kama haina tena hamu na sisi wanadamu kwani tumejikuta tukifanya mambo ambayo hata wanyama ni aghalabu sana kufanya.

Matukio ni mengi sana hata mengine hayafai kuandikwa hapa thesuperstars tz imekuwa ikipokea picha za uchi za wake za watu na waume za watu ambao hupigwa na mahawara zao kwa lengo la kutaka penzi au pesa na anapokosa huzivujisha picha hizo kwa vyombo vya habari.

Ila habari hii imenistua kidogo kwani  mwanamke huyu asiyekuwa na hata chembe ya aibu aliamua kuzitundika picha zake kwenye mtandao wa facebook kwa madai kuwa mumewe hayupo na wala hana mpango na facebook kwa hiyo hawezi kuziona picha hizo chafu na zinazotia kinyaa,ambazo zimeshuhudiwa na thesuperstarstz na kushindwa kuziweka hapa.

Kitu cha kujiuliza ni kwamba hata kama huyo mwanume haingii facebook inamaana hana marafiki au ndugu ambao wapo facebook wakamuambia anayoyafanya mkewe? na kitu kingine hadi mwanamke tena mke wa mtu ufikie kuweka picha kama hizo unatafuta nini wakati umeolewa je unataka kumuonyesha nani mwili wako na una muonyesha ili iweje wakati mume wako yupo.

Baada ya kuona picha hizo the superstarstz ilijiunga urafiki nae hadi kufikia kupata namba ya simu na ilipomsomaea kesi yake kwanza alicheka bila wasi wasi na kusema Nikuambie kitu kaka hizo picha ni zangu kweli lakini wala sijapiga kwa lengo baya ninapenda sana kupiga picha za nusu uchi na kama sheria ingeruhusu ningepiga za uchi kabisa kwani ndio hobi yangu  the superstarstz haikuishia hapo ilitaka kujua kama mumewe akiziona itakuwaje mwanamke huyo alijibu kwa kujiamini Kwanza mume wangu hayupo na wala haitaki facebook na hawezi kuziona na akiziona au akiambiwa hapo nitajua cha kufanya ila kwa sasa sina jibu kwasababu hajaziona

Haya wadau hayo ndio mambo ya mitandao au kifupi ni digital siku hizi hakuna mwana mke wala mwanaume wote wanatafutana cha muhimu kama hujafikia maamuzi ya kuowa au kuolewa usijiingize katika ndoa kwani utajikuta unafanya mambo ya ajabu kwakuwa hukuwa tayari kwa ndoa.