Tuesday 15 July 2014

IDADI YA WANAUME WAVIVU MWAMBAONI YAONGEZEKA NA NDOA NYINGI MATATANI

Na pengine ndilo hasa linalochangia ndoa nyingi kuvunjika na pengine imewafanya wanawake wengi kubakia ma single. Katika tamaduni zetu, mwanaume siku zote ndiye provider wa familia.
Anafanya matumizi ya kila kitu kinachofanya familia iendelee kuishi vyema, Chakula na kulipa mahitaji. Mwanamke yeye kazi yake ni kuakikisha nyumba inakuwa safi na familia siku zote inapata chakula.

Lakini sasa mwanaume wa kiafrika amekuwa na mawazo ya kimasikini, kwamba mwanamke naye alete chakula na kulipa mahitaji. Hii inawapelekea baadhi ya wanawake kubaki masigle kuliko kuolewa. Kama anaweza kulipa mahitaji, kutafuta chakula kama mwanaume. Anakuwa na uwezo wa kuishi peke yake labda atampata mmoja temporarily wa kumzalisha. 


Wanawake pia wamegundua kwamba, ni vyema kuchukuwa jukumu la Mama na Baba katika kulea watoto wao kuliko kuteseka na ndoa ya mwanaume mvivu kisa tu kuwa na figure ya mume. Ambaye yuko pale kwa ajili ya watoto.

Ni changamoto tu, wanaume tufanye kazi. Za mikono na akili