Sunday 13 July 2014

"MPENZI TUJENGE NYUMBA MBILI TUKIACHANA KILA MTU ACHUKUE YAKE"




Chonde jamani baadhi ya kina mama/dada/wasichana mbona mna roho kama za ajabu hivi.


Unawezaje kumwambia mumeo tena wa ndoa maneno kama hayo? mweeee!


Maneno haya kaambiwa mwanaume na mkewe wa ndoa wiki moja iliyopita.


Kwa sasa jamaa hamuamini kabisa mkewe akihofia huenda huyu mwanamke atakuja kumuua kwa sababu ya mali.


Wakiwa sebuleni baada ya kula mwanamke-ghafla tu-akamwambia mumewe eti wajenge nyumba nyingine ya pili ili ikitokea huko mbeleni wakiachana basi kila mmoja awe na nyumba yake kwani hii nyumba wanayoishi sasa mwanaume alijenga kabla ya kumuoa yeye.

Mwanamke anahofia hatapata kitu ikitokea atakufa au wakiachana huko mbeleni.

Mshikaji kaja niambia afanyeje, maana anahofia huenda huyu mwanamke anaweza kuja kumtoa roho kama watakuja kuwa na mali.


Sababu ya hofu hii, mshikaji anafikiria hata kukiuza kiwanja chake kilichopo bunju alichokuwa anapanga kuanza ujenzi mwezi wa nane.


Hivi jamani mkeo akikwambia maneno kama haya, na ndo hivyo ushamuoa kwa ndoa ya kanisani utafanyaje?