Ili Uhusiano au Ndoa iwe yenye furaha inahitaji Nguzo kuu 5 ambazo ni Maelewano/Makubaliano, Mawasiliano, Heshima, Uvumilivu na Ushirikiano....Mengine yote hujitokeza humo.
Nguzo moja kati ya hizo ikikosekana hakika Ndoa au Uhusiano utayumba. Sasa mmoja asipotoa Ushirikiano kwenye Mawasiliano ili kuwe na Maelewano, amani na furaha hutoweka.
Hata kama unayajua sana Mambo kitandani, huwezi kuendelea kuishi na mtu asiekupa ushirikiano, asie kuheshimu, kukupenda n.k. Kama umejitahidi kufanya yote au mengi uliyofundwa kama mke lakini Mume haonyeshi kuelewa au kutaka kubadilika ili muendelee kufurahia Muungano wenu then ni bora kutoka Ndoani.Hivyo nadhani hao Makungwi ndoa zao zimefeli kwa sababu nyingi tofauti lakini wapo ni kutokupata ushirikiano kutoka upande wa pili.
Kwasababu mwanamke kafundwa haina maana ndio awe mtekelezaji wa mahitaji yote muhimu kwenye Ndoa.
Ndoa ni umoja, Ndoa ni Timu....ndoa ni kuwa tayari kujifunza na kubadilika inapobidi ili muendane