Friday 11 July 2014

Maamuzi Gani Nichukue Dhidi ya Ndoa Yangu?

Mimi ni mama wa watoto wawili, nimefunga ndoa miaka saba iliyopita,
mwanzo kabisa maisha yangu ya mahusiano hayakuwa mazuri hata kidogo,
first of all niliwahi kubakwa nikiwa na umri wa miaka 15, baada ya
hapo niliishi maisha ya tabu sana mpaka nilipokuwa mkubwa na kuweza
kujitambua.Nillianza maisha ya mahusiano nikiwa na miaka 21 na

mwanaume niliyetokea kumpenda na kuamini yeye ndioatakayenifuta
machozi na huzuni zangu.Mambo hayakuwa hivyo kwani miaka miatatu ya
mahusiano yetu alienda oversizi na kuniacha na pia kuamua kukata
mawasiliano kabisa. Nilibaki na kovu na maumivu niliyokosa tiba.
Nilimtafuta bila mafanikio na kuamua kumove on na maisha yangu,ingawa
ilikuwa ni ngumu sana.Baada ya hapo nilikutana na mwamaume ambaye
sikujua kama ni kweli nampenda kwani siku zote nilipokuwa nae nilikuwa
namuwaza X wangu aliyeniacha bila kusema neno lolote.Mwanaume huyu
mwanzo sikumuelewa kabisa kwanza alikuwa mgomvi na mkorofi kwawatu
dakika mbili alishabadirikahaeleweki kama kinyonga,police kwake
ilikuwa ni kama nyumbani.Nyimbo zake mara nyingi zilikuwa ni za kina
Tupac ,SnopyD na wale aina ya magang star Ingawa alikuwa msomi na kazi
nzuri,na maisha yake mpaka sasa
bado miziki yake ndio hiyo,starehe
kwake hataki kuacha wala kupunguza.Niliamini atabadilika ingawa
nilikuwa nakwazika sana kuwa nae alinifundisha kunywa Pombe ,Ok nikawa
mnywaji mzuri na ili niwe nae Kimapenzi niliona ninywe kwanza ndio
nakuwa huru na hayo ndio yakawa maisha yangu..Tuliendelea na mahusiano
ya muda mrefu hatimaye nilianza kumzoealakini si kumpenda ,Tukiwa
tayari ndani ya mahusiano nilishika mimba na tukakubaliana kuanza
kukaa pamoja ,taratibu za mahali zilifanyika na nikahama rasmi lakini
kwa sababu jamaa alikuwa mtu wa starehe alikuwaakiniacha na kurudi
usiku wa manane amelewa mara anitukane na sikuona kama alikuwa
ananithamini na hali yangu ya ujauzito chuki moyoni ikawa inazidi siku
hadi siku.Ingawa kuna wakati nilikuwa naona kama ananipenda .Baadaya
kujifungua tulianza taratibu za ndoa lakini moyoni mwangu nikijua
kabisa mwanaume huyu sina mapenzi nae hata kidogo.Na nilikuwa
najiuliza kwanini nafunga ndoa? Ingawa kuna vitu vingine vilikuwa kama
najifosi kufanya. Tulifunga ndoa takatifu
nakuanza kuishi kama mke na
mme ,na mungu akatujaalia kuongeza mtoto mwingine wa kiume lakini
system yangu ni mpaka ninywe ndio nakuwa na hisia za kuwa na mme
wangu.Ndani ya ndoa yangu nimekuwanikiishi kwa kujifanya nampenda mme
wangu ingawa hizo hisia sijawahi kuzipata hata kidogo ,nimekuwa
nikilia na kujutia maamuzi yangu sina furaha ,ni mnyonge ,for the sake
of my kids ndio napata faraja kidogo.Kila siku zinavyoenda nazidi
kuchanganyikiwa mwenzenu nitaishi hivi mpaka lini nifanye nini ili
nipate amani ya roho,? maana hii pretend sasa imenichosha. Nakosa
usingizi usiku kucha.Ni mengi ya kuelezea lakini kwa hapa moyo wangu
unazidi kuwamnyonge Nisaidieni juu ya hili By Ndoa Yangu JF