Saturday 5 July 2014

Mfanyie mwanamke akuzidishie raha USIKU!!!


MAMBO vipi ndugu zangu? Ni furaha yangu kwa mara nyingine tena kukutana nanyi wapendwa wasomaji wa safu yetu hii.

Tumshukuru Muumba wetu kwa kutujaalia uhai na afya njema, lakini zaidi ya hapo tumshukuru pia kwa kutuumbia kitu mapenzi au siyo jamani? Siku zote hatutaacha kuzungumza juu ya mapenzi kwani ni ukweli usiopingika kwamba mapenzi ndiyo maisha yetu.
Tunafanya kazi usiku na mchana, tunahangaika huku na huko, lakini mwisho wa siku tunafikiria jinsi gani tutapata kuboresha na kufurahia maisha na wapenzi wetu. Tunafikiria pia ni jinsi gani tunaweza tukapata utulivu na amani katika maisha ya kimapenzi na wapenzi
wetu, waume zetu au wake zetu katika siku zote za maisha yetu. Ndugu zangu, Mungu ametuwekea mapenzi ili tupate raha na amani katika maisha yetu.

Kwa maana hiyo, wale wanaoyachezea na kuyavuruga mapenzi kwa makusudi kwa kuumiza hisia za wenzao kisha kuwasababishia vilio si watu wa kupendeza mbele ya macho ya wale
wanaojua hasa nini maana ya mapenzi.
Wanawake ni watu wa kuheshimika na kupewa furaha wanayohitaji. Unapompata mwanamke anayekupenda na kukuheshimu, huna sababu ya kumfanya ajute kuwa na wewe.