Saturday 5 July 2014

HUYU NDIO SUPER STAR BIKIRA KUTOKA NIGERIA ALIEWAAHIDI BOKO HARAM URODA WAKIWAACHIA WASICHANA WALIOWASHIKILIA

Muimbaji wa kike wa Nigeria, Adokiye Kyrian ambaye April mwaka huu alidai bado ni bikira na ataendelea kuwa hivyo hadi pale atakapopata mwanaume sahihi atakayemnunulia
mama yake ndege binafsi, amemake headlines tena kwa kuwaahidi Boko Haram uroda watakapowaachia wasichana 300 wanaowashikilia.
“Natamani kujitoa mwenyewe kwao,” alisema Adokiye Kyrian kwenye mahojiano na gazeti la Vanguard.

“Wana umri kati ya miaka 12 na 15. Mimi ni mkubwa na mzoefu kidogo. Hata kama nikitembea na wanaume 10 hadi 12 kila siku, sijali. Waachieni wasichana hawa na warudi kwa wazazi wao,” alisema.