Thursday 20 July 2017

JIBU la Aika (Navy Kenzo) kuhusu Jux na Vanessa Mdee kuachana

Msanii wa Bongo Flava kutoka kundi la Navy Kenzo, Aika amepata kigugumizi kuzungumzia taarifa za Jux na Vanessa Mdee kuachana.
Muimbaji huyu ambaye amekuwa rafiki wa karibu wa couple hiyo, alipoulizwa na 5 Sekt ya EATV alijibu, “sidhani kama hilo ni swali ambalo naweza kulijibu, wale ni wapenzi wana-relationship yao, mimi hainihusu kabisa ila naheshimu maamuzi yao,” amesema Aika.

Katika hatua nyingine Aika ametoboa siri ya uhusiano wake na Nahreel kudumu kwa muda mrefu, “sisi tuko real ikitokea kitu kwa siku moja ikavuma inakuwa ndio hivyo lakini tunajua jinsi ya kutatua matatizo yetu, tunajua jinsi ya kutulizana ikitokea tatizo, tunajua jinsi ya kuongea na kuhakikisha vitu kama watu wazima vinaishia ndani ya nyumba,” amemaliza kwa kusema.