Wednesday 26 July 2017

UJUMBE Mzuri siku ya Leo Kwa Ajili Yako Utakaokufungua Macho na Moyo

DARASA HURU
Kijana mmoja wa kiume alikuwa akipita nyumba moja hadi nyingine kulilisha tumbo lake lilokuwa na njaa, mwishowe akaamua kuomba chakula katika nyumba inayofuata. Lakini katika hiyo nyumba alishindwa kutimiza dhamira yake hiyo pale msichana mzuri alipofungua mlango. Hivyo badala ya kuomba chakula, akaomba glass ya maji. Msichana alipomtazama akamuona yule kijana anaonyesha ana njaa, hivyo akamletea glass kubwa iliyo jaa maziwa. Akayanywa taratibu, kisha akamu uliza yule msichana "unanidai kiasi gani kwa ajili ya hiki ulichonipa?" "Sikudai chochote. Mama ametufunza tusikubali malipo kwa tendo lolote la fadhila." Yule kijana akamwambia, "kwa hiyo ninakushukuru kutoka moyoni mwangu kote".
Miaka mingi ikapita, yule msichana (sasa ni mwanamke) alipata maradhi mabaya na madaktari wa sehemu ile walijaribu sana kumponesha lakini hawakuweza. Mwishowe wakaamua kumpeleka mjini ambapo madaktari bingwa watamchunguza. Dr Kelly ali itwa, na aliposikia mji yule msichana anapotoka, mwanga wa ajabu ukampata machoni mwake.
Mara moja aliamka akaenda chumbani akipolazwa yule mwanamke. Alimtambua mara moja. Alirudi ofisini kwake akaa mua kufanya kila awezalo kumponyesha yule mwanamke. Baada ya jitihada kubwa, alifanikiwa na yule mwanamke akapona.
Dr Kelly akaiagiza ofisi ya biashara kumletea bill ya mwisho ya yule mwanamke. Aliitazama bill ile, aka andika maneno machache kisha bill ile ikapelekwa chumbani kwa yule msichana. Mwanamke yule akawa anaogopa kuifungua ile bill akihofu itamchukuwa akiba yake yote aliyokuwa ameweka kulipa gharama za pale. Mwishowe alipofungua, akaona maandishi yaliyo andikwa chini yake "imelipwa kamilifu kwa glass ya maziwa"
Machozi yalimtiririka mara moja alipokumbuka. Tendo lolote la fadhila unalolitenda halipotei. Linajirudia. Sio lazima palepale lakini baadae hujitokeza. Nimekuwa mwema kukupa hadithi hii. Nawe kuwa mwema kuwapa wenzio. Ni vyema kuwa mwema. Kila mara kuwa mzuri : itakurejea.