Monday 31 July 2017

Sijamuona wa kushindana na Alikiba – Abdu Kiba

Msanii Abdu Kiba amemkingia kifua kaka yake, Alikiba wakati huu ambao mashabiki wanamuandama kuhusu kutoa ngoma mpya.


Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa hilo wanalichukulia kama changamoto ila kitu ambacho hawakipendi ni kuhusishwa na team za kimuziki au kuonekana wanajipanga kushindana na watu fulani.

“Sisi tunachukulia ni changamoto kwa sababu sisi hatushindani, tunafanya kazi na hatujaona bado wa kushindana nao, hakuna mtu wa kushindana na sisi, yaani sijamuona wa kushindana naye na hakuna wa kushindana na sisi na sisi hatushindani,” amesema Abdu Kiba.

Wiki iliyopita Abdu Kiba alikaririwa akisema ngoma mpya ya Alikiba ipo mbioni kutoka.