Thursday 27 July 2017

Waandamanaji wajenga ukuta kuzuia wakimbizi

Waandamanaji katika mji wa Séméac kusini magharibi mwa Ufaransa wamejenga ukuta unaozunguka lango la hoteli ya zamani kuzuia isitumiwe kama makao ya wahamiaji.


Wakazi wa eneo hilo waliweka ukuta wenye umbali wa mita 18 na urefu wa mita 1.8 unaozunguka hoteli hiyo ya Formule 1.

Waandamanaji hao wamesema mamlaka zimeshindwa kujadili mustakabali wa wahamiaji hao kwa kushindwa kuwapa makazi wahamiaji hao 85.

Hata hivyo bado Mamlaka husika hazijasema lolote kuhuhu ujenzi wa ukuta huo na Waandamanaji walifanya kazi hadi usiku kuweka ukuta huo.

“Hatupingi kuwachukua waandamanaji lakini lazima suala hili liwajibikiwe,” amesema Msemaji wa kundi hilo la waandamanaji Laurent Teixeira kwenye mahojiano yake na Reuters.