Wednesday 26 July 2017

Mabilionea 26 Watalii Waliokuja Serengeti kwa Kuvutiwa na Uzuri wa Tanzania

Siku za hivi karibuni headlines za mastaa kadhaa wa Soka, Muziki na Filamu Duniani kutembelea Mbuga za wanyama na vivutio mbalimbali vya Tanzania zilishika kasi licha ya mastaa hao kuingia kwa siri kwa ajili ya mapumziko.

Licha ya baadhi ya mastaa hao kuja kwa siri Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe amekutana na Watalii 26 ambao ni Mabilionea ambao wamewasili nchini kwa ajili ya kutembelea Mbuga ya Serengeti wakidai kuvutiwa na Tanzania kutokana na ubora wa Mbuga za wanyama.

Leo July 25, 2017 Ayo TV na millardayo.com zimezungumza na Waziri Maghembe:

“Wanatembelea nchi nane. Ni Mabilionea, Maraisi wa Makampuni. Kwa hiyo, wana Chama chao wakati wa likizo wanapenda kutembelea nchi kwa pamoja. Wakati huu wanatembelea nchi nane, walitembelea Uingereza, Rwanda na ya tatu Tanzania.

“Wakiondoka hapa wanakwenda Maldives, karibu na India halafu wanakwenda Nepal, Bhutan, Rajasthan. Ni watu ambao wamekuja Tanzania kwa ubora wake, kwa uzuri wake na wamekuja moja kwa moja Serengeti.” – Waziri Maghembe.