Thursday 27 July 2017

Aliyeshambulia watu kwa kutumia msumeno akamatwa

Polisi nchini Uswisi wamemkamata mtu ambaye anaaminika kufanya shambulizi la kigaidi kwa kushambulia watu kwa kutumia msumeno siku ya jumatatu.

Picha za usalama zikionyesha mshukiwa alivyokuwa akijiandaa na shambulizi hilo

Shambulizi hilo lilitekelezwa ndani ya ofisi moja ya umma na mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Franz Wrousis, 51 alishawahi kuwa mfanya kazi kwenye Ofisi hizo na lengo lake lilikuwa ni kuwateketeza wahudumu wote kwa kuwakata na msumeno wa moto (Chainsaw).

Baada ya tukio hilo, Franz Wrousis mwenye alimakatwa na askari kilomita 60 nje ya mji wa Schaffhausen ambako shambulizi hilo lilipotokea.

Wafanyakazi watano waliojeruhiwa kwenye Ofisi hiyo inayohusika na masuala ya Bima ya Afya hali zao sio vibaya, ingawaje mmoja hali yake inasemekana kuwa bado ni mbaya .