Monday 31 July 2017

KAULI Ambazo Ukizisikia Zinaashiria Uhusiano WENU Kuelekea Ukingoni.

Kuna kauli nyingi ambazo ukiwa kwenye uhusiano usingependa kumsikia mwenza wako akizisema.

Kauli kama “Inabidi tuongee” ni miongoni mwa kauli ambazo husababisha aliyeambiwa akose raha kwa muda wote anaosubiri mazungumzo hayo. Wakati mwingine, kauli kama hizi zisizoeleweka huwa ni viashiria tu kwamba ya kwamba jambo kubwa na la kutisha linakaribia kutokea kwenye uhusiano wenu.

Kwa kusema hivyo, hata kauli ambazo zinaweza kusemwa kiutani pia huweza kuwa na ishara mbaya kwenye uhusiano. Kama mwenza wako anasema mojawapo au zaidi ya kauli moja kati ya hizi zifuatazo mara kwa mara, basi ujue kwamba yawezekana wa kutafakari kwa kina uhusiano wenu na hatua za kufanya mapema:

“Sitakuangusha”

Kupeana ahadi ni jambo muhimu kwenye uhusiano lakini kama mpenzi wako anakuwa anaahidi au kuapa mara kwa mara kwamba hawatakuangusha kwenye uhusiano wenu kwa njia yoyote, ujue kabisa kwamba hapo unadanganywa wazi wazi.

Wewe ni lazima utakuja kumkosea na yeye pia atakukosea. Kama akiwa anasema tofauti na ukweli huu, ujue kwamba anaahidi kitu ambacho hamna mtu yeyote anayeweza kukitimiza au pengine ikawa moja kwa moja anamaanisha kwamba hata atakapokukosea itakuwa ni ngumu kwake kukubali kosa alilofanya.

Ni jambo la kawaida wapenzi kukoseana kwa sababu sisi sote ni binadamu, si wakamilifu – makosa yanatokea. Mara nyingi makosa haya si ya makusudi, lakini mara nyingine yanatokana na hasira tu. Usikubali ahadi za kitapeli za aina hii na ujipe nafasi ya kujenga uhusiano na mtu mwingine ambaye ni mkweli zaidi.

“Una hasira za haraka sana”

Mtu akisema kauli hii ni sawa na kuwa anamwagia petroli kwenye moto: kumwambia mtu kwamba ana hasira za haraka akiwa tayari amekasirika itafanya kumuongezea hasira alizo nazo.

Si hilo tu, kama mpenzi wako anakwambia hivi anamaanisha kuyapuuza mambo ambayo yawezekana wewe yanakuumiza sana na kuyageuza yaonekane kama ni hasira zisizo na ulazima wowote. Anakuwa anakupa ujumbe wa wazi kwamba hajali hisia zako kuhusu jambo fulani na anapuuza kama hajapenda jinsi ulivyolisema.

“Nitaacha [ulevi, kamari, matumizi mabaya…] kwa ajili yako”

Kama mpenzi wako ana kitanzi shingoni au tabia ambayo huipendi, hatakiwi kuapa kwamba ataiacha kwa ajili yako “kwa ajili yako.”

Kwa mtu, kuacha tabia ambayo haipendezi inatakiwa kuwa ni uamuzi wa maisha na si mahusiano yote yanayodumu muda mrefu na chaguzi maishani hazitakiwi kudumishwa kisa tu kwa uwepo wa uhusiano baina yako na mwenza wako.

Ingawa woga wa kumpoteza mpenzi wako kunaweza kukufanya kuahidi jambo kama hili, lakini ujue kabisa kuwa huwa ahadi za namna hii hazidumu. Unaweza kujizuia wewe tu kutosema kauli za aina hii, kamwe huwezi kumzuia au kumshawishi mwenzio

Na endapo utajikuta umeshaahidi jambo kama hili, basi kushindwa kutelekeza ahadi hiyo kutakuwa ni sababu kubwa ya kupoteza uaminifu.

“Chagua kimoja, mimi au…”
Vitisho huwa vinakera na vinatakiwa kutumika tu endapo hali imekuwa mbaya sana. Kama una wasiwasi wa kumuumiza mtu au kujiumiza wewe mwenyewe kwa tabia yako, basi mpenzi wako atakuwa na sababu sahihi kabisa ya kutumia hata vitisho ili kukufanya uache jambo hilo.

Lakini endapo mpenzi wako anaamua kutoa vitisho kama kukutaka uchague moja kati yake na: mbwa wako / kukuacha peke yako /familia yako, hiyo ni ishara ya kutodumu kwa uhusiano wenu na kwamba anachotaka ni kutawala maisha yako yote.

“Unatakiwa kufanya…”
Bila shaka wengi wetu tumefanya kosa hili la kuwaomba wapenzi wetu wafanye jambo fulani la ajabu kwa sababu yetu lakini wewe hutaki mpenzi wako akwambie vitu anavyotaka uvifanye.

Kama kweli anataka kukwambia ufanye jambo fulani, njia ya kidiplomasia zaidi ni angalau kwa kukuuliza swali akiomba ufanye jambo hilo na amri zake ziwe mwishoni kabisa kwenye dharura maalumu.

Hili lieleweke wazi: watu wazima hawaambiani lipi la kufanya, labda mkiwa kwenye uhusiano wa mmoja kumtawala mwenzake (kama uhusiano kati ya bosi na muajiriwa), lakini kama si uhusiano wa aina hii, hatakiwi kumwambia mtu mzima nini cha kufanya au kutofanya.

Kama mmoja anajaribu kumtawala mwenzie, hayo si mazingira sahihi ambapo mapenzi yanaweza kushamiri.

“Sikupendi”
Sote tunasema mambo ambayo hatuyamaanishi tunapokuwa na hasira lakini iwapo mpenzi wako anaelezea udogo wa hisia zake kwako kila mara kwa kukwambia kwamba hakupenda au anakuchukia, jua wazi kwamba hiyo ni ishara mbaya sana.

Ni rahisi sana kujikuta unaropoka kutokana na hasira ulizonazo na baada ya muda kujikuta unajuta, hata hivyo, kuelezea chuki ulizo nazo juu ya mtu wa muhimu zaidi kwako si jambo atakalokuja kulisahau maishani mwake na itaharibu uhusiano wenu kirahisi sana.

“Tuachane” (Inaposemwa kiutani)
Muda pekee ambao unatakiwa kusikia kauli ya “tuachane” inatakiwa iwe ni wakati ambao kweli uhusiano huo unakwisha.

Kama mwenzio anatishia “kuachana ” au anatishia kukatisha uhusiano wenu kutokana na mabishano madogo tu, kwamba yupo tayari kukufanya ujisikie kwamba hauna nafasi kwenye uhusiano wenu. Hiyo ni kukuonesha kuwa hajali maumivu unayopata au hadhani kwamba kuna uwezekano ukasema, “Sawa, tuachane tu,” mradi aonekane kuwa yeye ndiye aliyesema muachane kwanza.

Ingawa mapenzi huwa yanavunjika, kama huna nia ya kuachana naye basi usimtishie mwenzio kwamba mtaachana na kila mtu kwenda na njia yake. Woga wa kuachana na mpenzi wako na vitisho vya aina hiyo yanaweza kumsababishia mwenza wako msongo wa mawazo, hasa ikiwa mpenzi wako alishawahi kuachwa au akiwa na matatizo mengine ya afya ya akili.