Wednesday 26 July 2017

“Nikiondoka Hakuna Atakayekuwa Kama Mimi” – Kauli 7 za Rais JPM

Rais Magufuli leo July 25, 2017 ameendelea na ziara yake ambapo alikuwa katika Mkoa wa Singida alikozindua Barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa km 89.3 ambapo mbali na kufanya uzinduzi huo alipata nafasi ya kuhutubia wananchi.

Nimekusogezea mambo 7 makubwa kati ya mengi aliyozungumza kwenye hotuba yake.

'Pengine nikiondoka mimi hakuna atakayekuwa kama mimi, nasafisha njia ya Rais atakayekuja baada ya mimi' - Rais @MagufuliJP

'Ni lazima niyatapike yote haya, nikikaa nayo nitapata presha bure, ila wale walioyafanya wakumbuke na madhambi yao' - Rais @MagufuliJP

'Suala la ubinafsishaji mimi silipendi kabisa, siwezi nikawalaumu waliofanya hivyo lakini pia siwezi nikaacha kusema' - Rais @MagufuliJP

'Nataka Tanzania hii iwe kama Ulaya na tutafika tu, lakini ili tufike huko ni lazima tutabanana kweli kweli'- Rais @MagufuliJP

'Wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli waanze kujiandaa kisaikolojia, wanaweza tu kuanza kubomoa taratibu nyumba zao'- Rais @MagufuliJP

'Niliporudishwa wizara ya ujenzi nilimfukuza Chief Executive Officer ndani ya siku 3 kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha' - @MagufuliJP

Wengine mmewachagua lakini wanaongelea ya mambo Dar es salaam tu kosea kuoa unaweza kutoa talaka lakini usikosee kuchagua - Rais @MagufuliJP