Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameapishwa leo ikiwa ni wiki moja imepita tangia apate ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa Urais nchini humo.
Rais mpya wa Ufaransa ‘Emmanuel Macron’
Rais huyo mdogo zaidi kiumri kuwahi kutokea nchini Ufaransa tangu ‘Napoleon’ alimshinda pakubwa kiongozi wa chama cha mlengwa wa kulia Bi Marine Le Pen.
Bwana Macron, ambaye aliendesha siasa zake akiunga mkono umoja wa Jumuia ya mataifa ya Bara Ulaya, ameahidi kufufua uchumi wa Ufaransa na kufanyia mabadiliko siasa za kale za Ufaransa.
Hata hivyo Ili kufikia mabadiliko hayo chama chake kipya cha The Republic on the Move, kinatakiwa kushinda viti vingi vya ubunge katika uchaguzi wa mwezi ujao.
Wachambuzi wengi wa Masuala ya Kisiasa wanasema Rais Macron atafeli kuleta mabadiliko aliyoyaahidi kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake wa chama cha Kisosiolosti Francois Hollande, ambaye aliahidi mabadiliko, lakini anaondoka kama Rais asiye na umaarufu katika historia ya Ufaransa.
Rais mstaafu wa Ufaransa ‘François Hollande’ kushoto akiwa na Rais mpya ‘Emmanuel Macron’
Rais Emmanuel Macron akiapishwa leo Ikulu ya Ufaransa ‘Elysee’
Hapo akipokelewa na Rais mstaafu wa Ufaransa ‘François Hollande’
Picha zote kwa hisani ya Mtandao