Wednesday 31 May 2017

Diamond ashindwa kuhudhuria mazishi ya Ivan, Uganda

Baada ya Diamond Platnumz kutangaza kwamba angehudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga, ameshindwa kuhudhuria mazishi hayo yanayofanyika jioni hii katika makaburi ya ukoo wa marehemu yaliyoko Kayunga, nchini Uganda.

Zari akiwa na watoto wake

Muimbaji huyo weekend hii alishambuliwa na mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kutokana na kitendo chake cha kufanya show nchini Kenya licha ya mama watoto wake, Zari kufiwa na mume wake huyo wa zamani.

Meneja wa msanii huyo, Sallam amedai Diamond ameshindwa kuhudhuria mazishi hayo kutokana na ratiba kuingiliana.

“Kwenye mazishi hatujahudhuria, ilikuwa twende leo alfajiri lakini sasa kumbe wao wametoka usiku kwenda kijijini. Kwa hiyo nadhani ratiba yetu imeingiliana maana na sisi tulitoka Nairobi jana jioni.” Sallam alikiambia kipindi cha U-heard cha Clouds FM.

Pia Sallam amekanusha taarifa za kwenye mitandao ya kijamii kwamba wameshindwa kuhudhuria mazishi hayo baada ya kuzuiwa airport kuingia nchini Uganga kutoka na ishu za usalama.

Alisema wao walitaka kuhudhuria mazishi hayo kwaajili ya mkupatia pole Zari kwa kuwa huyo ndiye mtu wao.