Wednesday 31 May 2017

Wizara ya Fedha Yaliomba Bunge Sh 11.7 Tilioni..!!!!

Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge iliidhinishie Sh11.757trilioni ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote tisa yaliyo chini ya Wizara hiyo.


Maombi hayo yametolewa leo na Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni Mjini Dodoma.


Dk Mpango amesema kuwa kati ya fedha hizo, Sh10.328trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh1.429trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.


Amefafanua kuwa matumizi ya kawaida yanajumuisha Sh87.996bilioni kwa ajili ya mishahara, Sh778.6bilini kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC) na Sh9.4trilioni ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na Huduma nyingine.


Pia katika fedha za matumizi ya maendeleo, Sh1.382trilioni ni fedha za ndani na Sh46.1bilioni ni fedha za nje.