Wednesday 31 May 2017

Video: Mchezaji aliyefungiwa kwa kujaribu kumbusu mtangazaji

Mchezaji wa Tenisi Maxime Hamou, amefungiwa kushiriki michuano ya French Open mjini Paris, baada ya kujaribu kumbusu muandishi wa habari wakati wa mahojiano.



Hamou mwenye miaka 21 ambaye alikwa akihojiwa siku ya jumatatu na mtangazaji wa TV, Maly Thomas, baada ya kupoteza mchezo wake katika mzunguko wa kwanza katika michuano hiyo.


Mchezaji huyo alionekana akiwa amemshika mabega Maly Thomas, na shingo licha ya mwanadada huyo kukataa mara kwa mara. Baada ya tukio hilo kusambaa chama cha Tenisi nchini Ufaransa kimesema kitendo hicho ni cha kukemewa kwa nguvu.

Hata hivyo Hamou alamua kuomba radhi kwa Maly kwa kuandiaka “Naomba msamaha kwa Maly Thomas kama amejisikia vibaya au alishituka wakati wa mahojiano yalipokuwa yakiendelea”