Wednesday 31 May 2017

Barcelona yapata kocha mpya

Baada ya Kocha Luis Enrique kutangaza rasmi kuwa atastaafu kuifundisha klabu ya Barcelona hatimae klabu hiyo imemtangaza rasmi kocha wa zamani wa Athletic Bilbao, Ernesto Valverde kuwa kocha wao mkuu mpya.

Ernesto Valverde

Valverde ambaye aliwahi kuwa mshambuliaji wa zamani wa Barcelona,wiki iliyopita alitangaza kuwa anaondoka Athletic Bilbao baada ya kudumu klabuni hapo kwa takriban miaka minne.

Hata hivyo ujio wa kocha huyo umewavutia mashabiki wengi wa Barcelona duniani kote kwani ni moja ya makocha bora wa LaLiga.