Tuesday 30 May 2017

January Makamba Akana Kuutaka Uwaziri Mkuu...!!!

Waziri wa Mazingira, January Makamba amekana katu katu kuwa alichukia na kususa baada ya Rais Magufuli kumtosa katika nafasi ya Waziri Mkuu wa awamu ya tano.

Akitiririka mubashara, Makamba ametabainisha kuwa baada ya uchaguzi siku zote amekuwa akiomba asichaguliwe katika wadhifa huo mkubwa bongolala maana ungeweza kumharibia keria yake kwenye siasa.

Bado nina umri mdogo na nina safari ndefu sana kwenye siasa na kuwatumikia wananchi. Ukichaguliwa nafasi hizo kubwa ina maana unaua karia na huwezi kuendelea na siasa.