Tuesday 30 May 2017

Faida 4 za Kufunga Mwezi Huu Mtukufu wa Ramadhan..!!

Kwa mujibu wa dini ya kiislam tunakumbushwa kuwa kila muislam mzima na mwenye afya njema anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya kufunga chakula na kinywaji mcahana na kutwa sambamba na kujizuia kushiriki toka alfajiri hadi magharibi.

Pamoja na hayo, matendo hayo yatoba hupaswa kuendana na kuswali sana pamoja na kusoma quran kwa wingi.


Katika mwezi huu wa Ramadhani kadhalika inatakiwa kwa muislam kuwa mengi ya maneno yake yawe katika kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwani ni jambo ambalo linasaidia katika kuusafisha moyo wake na kuiboresha funga yake.


Mbali na hayo zipo pia faida nyingine za kufunga kama zifuatazo


1. Ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu alizotuteremshia na faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi siku ya mwisho.


2. Faida ya pili ya mfungaji wa swaumu ni kujizoesha kuwa na subira, yaani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mtu anajifunza jinsi ya kuwa mvumilivu na kustahamili njaa, kiu na matamanio ya kimwili.


3. Faida nyingine ni kuwa muadilifu na kujifundisha usawa baina ya masikini na tajiri.


4. Pia funga hutusaidia kiafya kwani huifanya mifumo kadhaa ya mwili nayo kupata wasaa wa kupumzika kwa mda fulani.