Wednesday 31 May 2017

Mkuu wa mawasiliano wa ikulu ya Marekani amwaga manyanga

Mkurugenzi wa mawasiliano wa ikulu ya Marekani (White House), Bw Mike Dubke ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ikiwa ni miezi miwili tuu iliyopita tangia ateuliwe na Rais Donald Trump.

Mike Dubke

Mike Dubke, ambaye ni mwanamikakati wa chama cha Republican aliyebobea, alipewa kazi hiyo mwanzoni mwa mwezi Machi kwa lengo la kujaribu kurekebisha baadhi ya vitu kwenye idara ya mawasiliano ya ikulu hiyo ikiwa ni sehemu ya mabadiliko aliyopendekeza, afisa wa habari wa White House Sean Spicer .

Mabadiliko hayo yametokea huku kukiwa na taarifa kwamba kuna migawanyiko katika kundi la maafisa wa mawasiliano White House.

Bw Dubke ameondoka kwa nia njema, kwa mujibu wa tovuti ya kisiasa ya New York Times ambayo ilikuwa ya kwanza kutangaza habari hizo.