Wednesday 31 May 2017

Wastara afunguka kwa Uchungu Kuhusu Zari Kutukanwa

Wastara afunguka kwa Uchungu Kuhusu Zari Kutukanwa:
From @wastara84 - Ukimuona nyani kazeeka na bado anaishi ujue kakwepa mishale mingi saana mtanisamehe kwa masamiati huu
Lakini mim ni mama sijawahi kusahau uchungu wa mwana na wala sijamsahau aliyenifanya niitwe mama lakini usiniulize kwanin sipo na niliyezaa nae ni mambo binafsi sana sio lazima kila mtu ajue
Lakini akifa nitaenda na ikibidi kulia nitalia sababu alikuwa na bado atakuwa baba wa watoto wangu.....
Lakini why why why mtu atukanweee weee asemwee kipindi kibaya cha uchngu na mawazo kama hiki hivi jamani mnajua kufiwa kweli wenzangu mbona hili la zari kutukanwa limenishinda kabsa kuvumulia...
Mtazameni huyo mtoto mdogo kwenye pic anamtazama babaake kwenye pic aliyoishika huku akitabasam utafikiri anasema baba upo umeenda kutembea siku moja utaludi tuu
Pangine
Ajui hta maana kufa ailewi aelewi maskini
Acheni basi fikirieni machungu yenu mpate hata robo ya maumivu wanayopata viumbe hawa #kufaanapesaavifanani
Pole wafiwa @zarithebosslady 
Mungu amlaze mahali pema ivan ameen